Mkurungezi wa Halmashauri ya msalala SIMON Berege Akiongea na vyomba vya habari ofisini kwake juu ya shutuma za Ubadilifu mratibu wa tasaf |
Mkurungezi wa Halmashauri ya msalala Simon Berege akiongea na waandishi wa habari |
KAHAMA .
HALMASHAURI ya Msalala wilayani Kahama,imemsimamisha kazi mara moja Mratibu
wa Mfuko wa Maendeleo ya Jamii (TASAF),Morris Oswago,baada ya kuwepo kwa kaya
hewa 153, katika Mpango wa kunusuru kaya masikini ndani ya halmashauri hiyo.
Mkurugenzi Mtendaji wa halmashauri hiyo Simon Berege,jana
aliwaambia waandishi wa habari ofisini kwake kuwa hatua hiyo imefikiwa baada ya
kubaini kaya hizo hewa kupewa fedha za Mpango huo na kusababishia serikali
hasara ya jumla ya shilingi milioni 30.076.
Berege alisema kuwa katika kufuatilia Mpango huo mapema mwezi
huu,iligundulika kuwa baadhi ya kaya ziilingizwa katika mpango huo bila
kuzingatia vigezo vilivyowekwa.
Akifafanua alisema kuwa katika kutekelezaji wa Mpango wa
Tasaf awamu ya tatu,awali jumla ya kaya 58,137 zilitambuliwa kuwa ni masikini
kwa kuzingatia vigezo vilivyowekwa kuzibaini.
No comments: