nduku cha sandaka ambapo wizi aliimba sandaka |
hili ndiyo kanisa ambalo wauumi wake wakati wa kusali jemba moja likachota sandaka |
Wakati mchungaji na waumini
wa kanisa la EAGT (JERUSALEMU) lililopo kata ya majengo wilayani Kahama
mkoani Shinyanga wakiwa katika maombi
mazito huku wakiwa wamefumba macho kama ulivyo utamaduni wa makanisa
yanayojiita kuwa ya kiroho muumini mmoja alitumia fursa hiyo kuchota fedha za
sadaka.
Tukio hilo la aina yake lililovuta hisia ya watu wengi
limetokea jumapili april 9 mwaka huu majira ya saa kumi na moja jioni wakati
mchungaji Gwamiye akiongoza maombi kwa waumini wake huku wakiwa wamefumba macho
ndipo muumini mmoja alijifanya anatoa
sadaka kasha kuchota shilingi 2,000 ndani nduku.
Mmoja wa waumini wa kanisa hilo ambaye hakutaka kutaja jina
lake alisema licha ya muumini huyo kudokoa shilingi 2,000, siku hiyo hiyo misa
ya asubuhi muumini huyo alidakwa na mashemasi wa kanisa hilo baada ya kuchukua
fedha isiyofahamika wakati alipoungana na waumini wengine kwenda kutoa sadaka
ambapo hata hivyo alisamehewa.
“Huyu jamaa anayejiita kuwa ni muumini wa kanisa hili siku
hiyo hiyo ya jumapili majira ya asubuhi alisamehewa na mashemasi wa kanisa hili
baada ya kuchukua kiasi cha fedha ambacho ambacho walisema ni kikubwa bila
kufafanua huku wakidai pengine alikosa fedha ya kujikimu kimaisha,” alisema
muumini huyo wa kanisa la EAGT Majengo bila kutaja jina.
Hata hivyo baadhi ya waumini walidai kushangazwa na kitendo
hicho cha vibaka kuanza kuingia katika nyumba mbalimba mbali za ibada kwa lengo
la kuiba sadaka bila kumwogopa mungu.
Naye mchungaji wa kanisa hilo Felix Gwamiye alidhibitisha
kutokea kwa tukio hilo kanisani kwake na kusema kuwa kwa sasa kuna wimbi la
vibaka wanaoingia ndani ya makanisa wakati maombi yakiendelea huku wakati
wakiwa katika maombi mazito wao ndipo wanapata mwanya wa kudokoa fedha za
sadaka.
Katika tukio hilo Gwamiye alitoa wito kwa makanisa ya
kipentekostal wilayani hapa kukaa chonjo na vibaka wanaoingia kanisani na
kujifanya ni waumini kumbe wanavizia sadaka za waumini.
“Mtuhumiwa huyo alikamatwa na mashemasi wakati alipomuona
akiiba hela za sadaka baada ya waumini kumaliza kutoa sadaka na kuanza maombi,
mimi kama kiongozi wa kanisa hili nimemsamehe lakini asithubutu kuingia katika
makanisa yoyote hapa Kahama maana waumini
wakiamua kufunga novena ya maombi laana itamsumbua,” alisema Gwamiye.
Hata hivyo katika mahojiano yake na gazeti hili muumini huyo
aliyejitamburisha kwa jina la Dismas Simoni(35) mkazi wa Kata ya Ushirombo
wilaya ya Bukombe mkoa wa Geita alisema kuwa ni shetani ndiye aliye mtuma na
kujikuta anadokoa kiasi hicho cha fedha na kumuahidi kiongozi huyo wa kanisa
kuteua watu wa kuongozana nao kwa ndugu yake hali ambayo ilimfanya Gwamiye
amsamehe.
“Mimi ni mkazi wa kata ya Ushirombo Bukombe huku Kahama
nimekuja kumtembelea kaka yangu anayeishi kitongoji cha Nyamhela kata ya
Mhongolo binafsi niseme nimepitiwa tu na shetani samahani sana kama mtanisamehe
naweza kurudisha hela niliyochukua asubuhi nah ii 2,000/= siewezi kurudia kosa
jamani,” alisema mtuhumiwa wa kuiba sadaka.
Mwisho.
No comments: