By: Mohab Dominic
on 04:13
/
|
MKUU WA MKOA WA SHINYANGA ZAINAB TELLACK AKIKABIDHI MASUKA MWENYEKITI WA HALMASHAURI YA MSALALA |
|
Mkuu wa mkoa akiangalia masuka yaliohadi kutoa katika vituo vya afya halmashauri ya msalala |
|
Mwenyekiti wa halmashauri ya msalala Mibako mabubu na Mkurungezi wa halmashauri ya msalala simon Berege wakipokea mashuka toka kwa mkuu wa Mkoa wa shinyanga |
|
Mashuka ya msaada katika vituo vya afya msalala |
|
Mkuu wa mkoa wa shinyanga Zainab Tellack
SERIAKALI mkoani Shinyanga imetimiza ahadi yake juu ya ujenzi wa
shule ya msingi Mhungula iliyopo katika Kata hiyo Halmashauri ya mji wa Kahama.
Akikabidhi mabati hayo zaidi 140 yaliyotolewa na mkuu
wa Mkoa huo Zainab Tellack, kwa mkurugenzi mtendaji wa halamsahauri hiyo
Anderson Msumba, Diwani wa Kata ya Mhungula Ignas Shabani
alimwambia mkurugenzi huyo kuwa mkuu wa Mkoa huo aliahidi kusaidia ujenzi
huo.
Aidha Diwani Shabani alieleza kuwa mabati hayo yamegawanywa kwa
shule mbili za Kata hiyo ambapo shule ya msingi Mhungula imepatiwa mabati 90
huku shule ya msingi Bukondamoyo nayo ikipatiwa mabati 57.
Akifafanua zaidi Diwani alisema licha ya kuipongeza serikali kwa
msaada huo lakini bado kuna changamoto zingine zinazoikabili Kata ya Mhungula
likiwemo suala la umeme,maji pamoja na miundo mbinu za barabaraba ambazo
hazijatatuliwa.
Akipokea msaada wa mabati uliotolewa na mkuu huyo wa Mkoa kutoka
kwa Diwani huyo mkurugenzi mtendaji wa Halmashauri hiyo Anderson Msumba
alimshukuru mkuu huyo wa Mkoa kwa msaada wake.
Msumba alisema kuwa licha ya mkuu wa Mkoa wa Shinyanga kufanya
ziara yake katika shule hiyo na kubaini changamoto hizo na Halmashauri ilikuwa
tayari imejipanga vyema katika kukabiliana na changamoto hizo ambapo alidai
kwamba kabla ya mkuu wa Mkoa kufika shuleni halmashauri ilitenga kiasi cha
shilingi milioni192 kwaajili ya ukarabati wa vyumba vya madarasa hivyo mchango
wake utasaidia kuzidi kuboresha.
Mwisho
|
Tag:
habari
matukio
MOHABMATUKIO.BLOGSPOT.COM's Admin
We are.., This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.
No comments: