headlines

    9:53 PM

sponsor

sponsor

Slider

  1. 1
  2. 2
  3. 3
  4. 4
Theme images by kelvinjay. Powered by Blogger.

Kimataifa Habari

habari

Habari Za Mastaa

Michezo

simulizi za kusisimua

» » » DC Amuweka Ndani Dk Mary Nagu (Mbunge wa Hanang -CCM )
 Mohab Dominic

 
Mbunge wa Hanang (CCM), Dk Mary Nagu  jana alishikiliwa kwa muda polisi baada ya kutokea vurugu katika kikao cha kamati ya siasa ya chama hicho.

Dk Nagu aliyewahi kuwa waziri katika wizara kadhaa wakati wa utawala wa Serikali za awamu mbili zilizopita, alishikiliwa kwa muda  na kuachiwa baada ya kuhojiwa.

Kamanda wa Polisi Mkoa wa Manyara, Francis Masawe alisema Dk Nagu alifikishwa kituoni kutokana na vurugu zilizoibuka kwenye kikao cha kamati ya siasa ya CCM Wilaya ya Hanang baada ya makundi mawili kujitokeza.

Masawe alisema baada ya mahojiano kufanyika na kuandika maelezo, kwa kuwa mgogoro huo ulikuwa ni mambo ya ndani ya CCM walimwachia.

"Taarifa ambazo nimepata ameachiwa baada ya kuandika maelezo na tayari walifikia makubaliano wenyewe," alisema.

Awali, mkuu wa wilaya hiyo, ambaye pia ni mjumbe wa kamati ya siasa ya wilaya, Sara Msafiri alisema: "Ni kweli amekamatwa lakini nipo kwenye kikao siwezi kuzungumza.”

Habari kutoka ndani ya kikao hicho, zimeeleza Dk Nagu alikamatwa kutokana na malumbano ya kupitisha wagombea wa uchaguzi ndani ya CCM.

«
Next
DARAJA LA FURAHISHA MWANZA LAKAMILIKA
»
Previous
MAMLAKA ZA AJIRA NCHINI ZAAGIZWA KUREKEBISHA TAARIFA ZA WATUMISHI WA UMMA WANAOTARAJIA KUSTAAFU ILI WAPATE STAHILI ZAO KWA WAKATI
Pages 22123456 »

No comments:

Leave a Reply