WAZIRI wa nchi Ofisi ya Makamu wa Rais
Muungano na Mazingira Mhe. Januari Makamba (Mb) ametengua uteuzi wa Mkurugenzi
Mkuu wa Baraza la Taifa la Hifadhi ya Usimamizi wa Mazingira (NEMC) na Wajumbe
wa Bodi ya Wakurugenzi ili kuongeza tija na kutekeleza kwa vitendo dhana ya
Ujenzi wa uchumi wa viwanda.
Kwa kuzingatia mamlaka aliyonayo
Waziri chini ya Sheria ya Mazingira kifungu cha 19 (2) anaweza kutengua uteuzi
wa Mkurugenzi wa Baraza hilo na wajumbe wake.
Akizungumza na vyombo vya Habari leo Jijini
Dar es Salaam Waziri Makamba amesema kuwa lengo la mabadiliko hayo ni
kuhakikisha kuwa kunakuwa na usimamizi na uzingatiaji wa Sheria ya
Mazingira na uharakishaji wa miradi ya maendeleo na uwekezaji hasa
ujenzi wa viwanda kama azma ya Mheshimiwa Rais John Magufuli inavyoelekeza.
Kufuatia mabadiliko hayo Waziri Makamba
amemteua Dkt. Elikana Kalumanga ambaye ni Mhadhiri katika Taasisi ya Usimamizi
na Tathmini ya Rasilimali Asili,Chuo Kikuu cha Dar es Salaam, kuwa Kaimu
Mkurugenzi Mkuu wa NEMC hadi Rais atakapoteua Mkurugenzi Mkuu.
“Utendaji wa NEMC umekuwa ukilegalega sana na
umekuwa hauridhishi na kumekuwepo na malalamiko mengi kutoka kwa
wawekezaji wa ndani na nje ya nchi kuhusu ucheleweshaji na urasimu
usiokuwa wa lazima katika mchakato wa tathmini ya athari kwa mazingira (EIA)”
Alisisitiza Mhe. Makamba.
Aliongeza kuwa ametengua uteuzi wa wajumbe
wote saba wa Bodi ya NEMC ili baadaye ateue wajumbe wapya ambao wataendana na
kasi na ari ya Serikali ya Awamu ya Tano katika kuelekea uchumi wa Viwanda,
ambapo Mwenyekiti wa Bodi ambaye mamlaka yake ya uteuzi ni Mheshimiwa
Rais,ataendelea kuwepo hadi Mheshimiwa Rais atakapoteua mwingine.
Mwisho
Akifafanua Makamba amesema kuwa changamoto
nyingine zilizobainika ni kuwaelekeza wawekezaji kwa makampuni ya kufanya
Tathmini ya athari za mazingira ambayo yanamilikiwa au yenye ubia na watumishi
wa NEMC, bila kujali mgongano wa kimaslahi jambo ambalo haliruhusiwi katika
utumishi wa umma.
Jambo jingine ni kuwarundikia maandiko ya
miradi ya tathmini ya athari kwa mazingira (EIA) watumishi wachache wakati
wengine hawana kazi ili waelekeze miradi hiyo katika makampuni ambayo baadaye
huwapatia malipo yasiyo halali.
Hatua nyingine zilizochukuliwa na Waziri
Makamba ni pamoja na kuiagiza NEMC kufuta watu binfsi na Makampuni yote ya
ushauri wa EIA (Consultants) ambayo hayana sifa au yameshindwa kutekeleza kazi
zao vizuri na watangaze kwenye magazeti orodha ya watu na makampuni
yanayoruhusiwa kufanya kazi kama washauri elekezi.
Baraza la Taifa la Hifadhi na Usimamizi wa
Mazingira NEMC ni muhimu katika kuhakikisha ustawi wa mazingira na mustakabili
wa maendeleo endelevu ya nchi tunapoelekea kuwa Taifa la uchumi wa viwanda
lazima usimamizi wa mazingira uwe thabiti FRANK MVUNGI –MAELEZO
. mwisho
|
No comments: