Marekani na China zimekamilisha mkutano wa kibiashara kuhusu maswala tata mjini Washington bila maafikiano. |
Pande zote mbili hazikutoa taarifa ya pamoja ama hata mpango
baada ya mkutano huo na kufutilia mbali mikutano na vyombo vya habari
iliotarajiwa kufanyika.
Marekani ilikosoa biashara ya China na kutaka makubaliano ya
kibiashara ambayo hayatapendelea upande mmoja.
Rais Donald Trump amesema kuwa ushuru kuhusu vyuma vya China
bado huenda ukatekelezwa.
Katika hotuba yake ya ufunguzi wa mkutano huo wa kibiashara kati
ya mataifa ya China na Marekani, katibu wa biashara nchini Marekani Wilbur Ross
aliikosoa biashara ya ziada ya China yenye thamani ya dola bilioni 347 akisema
kuwa haitokani na mvutano wa kisoko.
Katika taarifa fupi, bi Ross na katibu katika wizara ya fedha
Steven Mnuchin alitoa maelezo machache na ishara kuhusu hatua zilizopigwa
kuhusu maswala tata.
''China ilitambua kwamba pendekezo letu la kupunguza tofauti ya
kibiashara kati ya pande zote mbili litaafikiwa'', taarifa hiyo ilisema.
Swala tata la kodi itakayotozwa vyuma vya China lilitarajiwa
kuwa mjadala mgumu katika mkutano huo, lakini pande zote mbili hazikutoa
taarifa yoyote.
Marekani inalaumu biashara ya ziada ya vyuma vya China ambayo
inaathiri wazalishaji wa Marekani na sasa imeonya kuweka kodi.
Kampuni za kuuza vyuma nchini Marekani hazikufanya biashara
nzuri huku wawekezaji wakidhani kwamba Marekani huenda ikaitoza kodi China kwa
biashara ya ziada ya vyuma vyao vinavyoingia Marekani.
Baada ya soko kufungwa, rais Trump aliwaambia maripota kwamba
kodi ya vyuma inaweza kutekelezwa kulingana na chombo cha habari cha Reuters.
No comments: