sponsor

sponsor

Slider

Theme images by kelvinjay. Powered by Blogger.

Kimataifa Habari

habari

Habari Za Mastaa

Michezo

simulizi za kusisimua

» » » Rais Magufuli aagiza Sh200 milioni za mradi wa maji jeshini zitumike kwa wananchi

John Magufuli ameagiza Sh 200 milioni zilizopangwa kutumika katika mradi wa maji katika kambi ya jeshi zianze kuimarisha miradi ya maji kwa wananchi kwanza.

Akizungumza leo, Alhamisi Julai 20 katika ziara yake akiwa ameambatana na Rais wa Burundi, Pierre Nkurunzinza, Magufuli amesema amebaini kuwa pampu za maji wilayani Ngara zimeharibika kwa zaidi ya wiki tatu na kuwa wilaya hiyo ina uhaba mkubwa wa maji.

Alimuita, Mhandisi wa Maji ajieleze ni kwa nini pampu hizo hazifanyi kazi na baada ya kumsikiliza ndipo alipofanya uamuzi huo.

Akifafanua kuhusu hali ya maji, mhandisi huyo amesema awali visima vya maji wilayani hapo vilikuwa vikihudumia watu 400 lakini kwa sasa wilaya hiyo ina watu zaidi ya 240,000 na hivyo visima hivyo havitoshelezi.

“Tulikuwa tuna idadi ndogo ya watu sasa hivi imeongezeka, lakini tangu pampu iharibike, tumetengeneza mbili na kisima kimoja hakina pampu,” amesema.

Baada ya mhandisi huyo kufafanua hayo ndipo Rais alimuita Mkurugenzi wa Halmashauri kueleza mipango yake, ndipo Mkurugenzi huyo aliposema mradi wa maji wa Sh 200 milioni utaanza kwanza katika kambi ya jeshi.

Kauli hiyo ndiyo iliyomfanya Rais Magufuli kushauri fedha hizo zitumike katika miradi ya maji katika makazi ya wananchi kwanza.

“Wanajeshi wapo 200 na wananchi wapo zaidi ya 20,000 sasa si bora waanze wananchi kwanza,” amesema.
   


«
Next
Newer Post
»
Previous
Older Post

No comments:

Leave a Reply