headlines

sponsor

sponsor

Slider

  1. 1
  2. 2
  3. 3
  4. 4
Theme images by kelvinjay. Powered by Blogger.

Kimataifa Habari

habari

Habari Za Mastaa

Michezo

simulizi za kusisimua

» » Amba Lulu Afunguka Pona Yake kwa Waziri Shonza
 Mohab Dominic

Amba Lulu nAfukunguka Pona Yake kwa Waziri Shonza

Amba Lulu Afunguka Pona Yake kwa Waziri Shonza


Amber Lulu amedai kuwa rungu la kuitwa na Naibu Waziri wa Habari, Sanaa utamaduni na Michezo, Mh. Juliana Shonza ni kutokana na kuwa watu walishamtoa kwenye kundi la wakaa utupu mitandaoni na kumuweka kwenye kundi la wasanii.


Kupitia 5Selekt ya EATV  Amber Lulu amesema kwamba baada ya kuingia kwenye muziki aliamua kufuta picha zote ambazo hazikuwa zikimtambulisha kama msanii.

"Mimi nimeshatoka kwenye lile kundi. Sikutajwa kwasababu watu wameshanitoa  kabisa kwenye Amber yule na wanamjua huyu wa sasa ambaye anaimba. Hata kwenye mitandao yangu ya kijamii ukipitia hutakutana na picha za miaka ile" Amber Lulu.

Amber Lulu aliingia rasmi kwenye sanaa ya muziki mwishoni mwa 2016,  akiachana na sanaa ya upendezeshaji wa nyimbo za wasanii 'Video Vixen'.

Hivi karibuni Msanii wa karibu na Amber Lulu aliitwa na Naibu Waziri Shonza kwenda ofisini kwake kutokana na kuvunja maadili kwa kupiga picha za utupu  na kuziweka katika mitandao yake ya kijamii.

«
Next
Maskini Johari! Apata Pigo Afiwa na Mama Yake Maskini Johari! Apata Pigo Afiwa na Mama Yake
»
Previous
Wasichana Waliotekwa na Boko Haram Wagoma Kurudi Nyumbani Wasichana Waliotekwa na Boko Haram Wagoma Kurudi Nyumbani
Pages 22123456 »

No comments:

Leave a Reply