sponsor

sponsor

Slider

Theme images by kelvinjay. Powered by Blogger.

Kimataifa Habari

habari

Habari Za Mastaa

Michezo

simulizi za kusisimua

» »Unlabelled » EWURA YATAKIWA KUDHIBITI UJENZI HOLELA WA VITUO VYA MFUTA KAHAMA



Na  Mohab Dominick
Kahama
Oct 28 2013.
 

MAMLAKA ya udhibiti wa nishati na maji (EWURA) imetakiwa kuangalia upya sheria ua jengwaji wa vituo vya mafuta katika maeneo mbalimbali hususani Wilayani Kahama ambapo vituo hivyo vimekuwa vikijengwa  ovyo hadi katika maeneo ya makazi ya watu.

Hayo yalisemwa na Katibu Tawala wa Wilaya ya Kahama Ernest Masanja kwa niaba ya Mkuu wa Wilaya ya Kahama Benson Mpesya katika kikao cha taftishi ya kujadili ombi la kurekebisha bei za huduma za Mamlaka ya maji safi na usafi wa mazingira (KUWASA).

Masanja alisema kuwa kwa sasa kumekuwa na mrundikano wa vituo vya mafuta ambavyo vimekuwa vikijengwa ovyo hadi katika makazi ya watu hali ambayo inaweza kuleta madhara makubwa  inapotokea ajali.

Alisema kuwa katika Mji wa Kahama kwa sasa vituo hivyo vimejengwa hadi katika makazi ya watu na kuwataka viongozi wa Mamlaka hiyo ya kudhibiti wa Nishati na maji kuangalia sheria upya inasemaje ili kuweza kudhibiti ujenzi huo ambao umekuwa kero katika Wilaya .

Kwa upande wake Mwakilishi wa Mkurugenzi wa EWURA George Kaberwa alisema kuwa suala amelichukua na kuhaidi kuwa atalifikisha katika ngazi husika kwa ajili ya kufanyiwa kazi na majibu yatatolewa muda utakapowadia.

Nae Meneja wa Mamlaka ya maji safi na usafi wa mazingira Wilayani Kahama (KUWASA) Joel Rugemarila akizungumzia kuhusu angezelo la Bei ya Maji katika Mkutano huo ambo ulijumuisha wadau wa maji alisema kuwa ametoa mapendekezo ya kuongeza bei za kutoka shilingi 595 hadi 970 kwa matumizi ya myumbani.

Rugemarila alisema kuwa kwa kuongeza bei hizo za maji kutasaidia kwa mamlaka yake kuweza kuwa na uhakika wa kununua maji kutoka kwa wauzaji wake ambao ni Mamlaka ya maji safi na maji taka Kahama na Shinyanga (KASHWASA).

Pia kutasaidia katika kuwa na uhakika wa maji masaa 24 na kuhakikisha kuwa mtandao wa maji unawafikia walaji wake kwa muda muafaka na watu wengi hasa katika maeneo ya mbali ambayo watu wanaishi.

Katika kikao hicho ambacho hata hivyo hivyo wadau hao wa maji ambao kwa asilimia 51 ni wakazi wa majumbani wakalikataa mapendekezo hayo kupandisha bei ya maji na kuitaka mamlaka hiyo kuangalia vyanzo vyake vya fedha na kuongezea na sii kumchangisha mlaji ambaye sii kazi yake.

mwisho

«
Next
Newer Post
»
Previous
Older Post

No comments:

Leave a Reply