sponsor

sponsor

Slider

Theme images by kelvinjay. Powered by Blogger.

Kimataifa Habari

habari

Habari Za Mastaa

Michezo

simulizi za kusisimua

» »Unlabelled » KASHWASA YADAIWA BILION 1.7 NA TANESCO



Na  Mohab Dominick
Kahama
Oct  22, 2013.




MAMLAKA ya maji safi na Maji taka Kahama na Shinyanga (KASHWASA) inadaiwa jumla ya shilingi bilioni 1.7 na shirika la umeme nchini Tanesco kutokana na kuchelewesha malipo ya bili za umeme unaendesha  Mradi wa maji wa Ziwa victoria katika miji hiyo miwili.

Hayo yalisemwa juzi na Meneja utawala na Rasilimali wa Kashwasa Denis Mulingwa katika kikao Mkutano wa Taftishi wa wadau wa maji wa kurekebisha bei za maji na huduma za mamlaka maji safi na usafi wa mazingira Wilayani hapa (KUWASA)

Mulingwa alisema kuwa kiasi shilingi bilioni 1.3 serikali haijazitoa kama Ruzuku kwa mamlaka hiyo na hivyo kusababisha kuwawia vigumu katika kulipa bili za umeme unaoendesha mradi huo mkubwa mkubwa kabisa ulioigharimu serikali kiasi cha shilingi bilioni 254.

Aidha Mulingwa aliendelea kusema kuwa sasa Mamlaka za Serikali hazina budi kubadilisha mfumo wa utendaji wa kazi kwa kutegemea Ruzuku za Serikali kwani kwa kufanya hivyo kutafanya kazi nyingi kusimama hali ambayo itazitia hasara mamlaka husika.

Alisema kuwa kwa Kashwasa imepata mfadhilia ambaye atawakopoesha kwa ajili ya kuondokana na deni hilo na kuongeza kuwa wao watatafuta mbinu nyingine za kuresjesha fedha hizo kuliko kusubiri Ruzuku hiyo kutoka Serikali kwani kazi zitasimama.

Aidha Meneja huyo alisema kuwa kwa sasa mashine moja kati ya tatu katika mtambo wa kusafirisha mji kutoka katika chanzo cha Ihelele imesimama na kuongeza kuwa kama hiyo moja nayo ikisimama basi huduma ya maji inaweza kusimama hadi kuagiza vipuri hivyo kwa oda kutoka China au Afrika ya kusini.

Katika Mkutano huo ambao ulijumuisha Wadau wa maji wengi wao wakiwa wale wa matumizi ya nyumbani waligoma kupitisha mapendekezo hayo ya kuongeza bei za maji na kuongeza kuwa mamlaka husika yaani kuwasa itafute vyanzo vingine mbadala ya kuwaingizia fedha na sii mlaji wa maji.

Wakichangia katika mkutano huo Diwani wa kata ya Kahama Mjini Abbasi Omary alisema kuwa mamlaka hiyo aiwezi kuongeza bei za maji huku viongozi wake wakitumia fedha zaidi ya mamilioni katika suala la mawasiliano pamoja na mafanyakazi anapofariki.

Alisema kuwa kutoka bei ya shilingi 595 hadi 970 ambacho kuwasa inataka kupandisha ni kikubwa na kuongeza kuwa bei hiyo hawezi kumudu mwananchi wa hali ya chini kwani wao wanajukumu kubwa la kubuni vyanzo mbadala vitakavyoisadia mamlaka hiyo na kuweza kujiendesha Mwenyewe.

Kwa upande wake Meneja wa Mamlaka hiyo Joel Rugemalila alisema kuwa katika mamlaka yake wametenga fedha hizo kwa ajili ya mawasiliano pindi inapotokea bomba limefaribika sehemu na hivyo kupeleka huduma mara moja na pia wananchi wanapotoa taarifa za wizi wa vifaa au kupasuka kwa bomba.

M wisho
                                    

«
Next
Newer Post
»
Previous
Older Post

No comments:

Leave a Reply