sponsor

sponsor

Slider

Theme images by kelvinjay. Powered by Blogger.

Kimataifa Habari

habari

Habari Za Mastaa

Michezo

simulizi za kusisimua

» »Unlabelled » WANAFUNZI WAWILI WA KIKE KUFANYA MTIHANI WA KIDATO CHA NNE SEKONDARI MWERINa  Mohab Dominick
 Kahama
0cto 28,2013.

 
KATIKA kuhakikisha Wanafunzi wa kike wanapata elimu sawa na wale wa kiume hali imekuwa kinyume katika shule ya sekondari ya Mweri Wilayani hapa ambapo jumla ya wanafunzi wa kike 48 walioanza kidato cha kwanza kwa mwaka huu katika shule hiyo lakini mpaka kufikia hivi sasa ni wanafunzi wa wawili tuu wa kike wanatarajia kufanya mtiahani wa kidato cha nne.

Hayo yalisemwa juzi wanafunzi wa Shule hiyo katika Risala yao  mbele ya Mdau mkubwa wa Elimu Wilayani Kahama Eliasi Ku
andikwa katika mahafali ya sekondari hiyo iliyopo katika kata ya Ushetu Wilayani hapa.

Katika Risala yao hiyo Wanafunzi hao pia waliwaomba wazazi kuwa na utaratibu wa kufuatilia maendeleo ya Wanafunzi katika shule hali ambyo inaweza kuchangia mahudhuri ya wanafunzi kuongezeka hasa kwa wanafunzi wa kike ambao ndio imekuwa tatizo kubwa shuleni hapo.

Walisema kuwa katika shule hiyo jumla ya Wanafunzi 70 waliopo katika shule hiyo wa kidato cha nne walianza kidato cha kwanza kwa mwaka huu huku wsasichana wakiwa 22 lakini hadi kufikia hivi sasa ni Wanafunzi wa kiume 20 na wa kike wawili ndio wanatarajia kufanya mtihani wa kumaliza kidato cha nne kwa mwaka huu.

Kwa upande wake Mgeni rasmi katika mahafali hayo Elias Kuandikwa alisema kuwa kama mzazi atatimiza wajibu wake  katika jamii basi hakuna mtoto wa kike atakayekosa Elimu  kwa ajili ya mzazi kutokuwa na karo au sare ya nguo za shule.

Kuandikwa aliwataka wazazi na Walezi katika kata hiyo ya Ushetu kuhakikisha kuwa wanafuatilia maendeleo ya Wanafunzi wao hasa wale wa kike na kuongeza kuwa ni jambo la ajabu kwa wazazi kuwa na visingizio vingi wakati kumsomesha mwanafunzi ni jukumu lao la msingi. Kuandikwa aliendelea kutoa masikitiko yake kuwa ni  aibu  wazazi wenzangu kijiji kizima na kata yaUshetu  kwa ujmla  kuona ni wanafunzi wawili tu ndio wanatarajia kumaliza kidato cha nne kwa mwaka huu  na kuongeza kuwa hii ni fedhea kwa jamii nzima ya hapa.

Akisisitiza juu ya Suala la Elimu kwa sasa hapa nchni Kuandikwa alisema kuwa Elimu kwa jamii kwa sasa kuna wajibu mkubwa  wa pamoja kati ya watendaji wa serikali ya kijiji na wananchi kujua wajibu wao kila moja ili tuwakomboe watoto wa kike katika taifa hili.

“Hakuna kitu kizuri kama kuwa na moyo wa umoja katika kuleta maendeleo na ni ngumu sana kama hatutakuwa na umoja katika utendaji na kushilikiana na serikali katika suala zima la Elimu na kuwakomboa watoto wetu hasa wa kike waliopo katika majarubu mengi wawapo mashuleni”, anasisitiza Kuandikwa.

Mwisho.

«
Next
Newer Post
»
Previous
Older Post

No comments:

Leave a Reply