sponsor

sponsor

Slider

Theme images by kelvinjay. Powered by Blogger.

Kimataifa Habari

habari

Habari Za Mastaa

Michezo

simulizi za kusisimua

» »Unlabelled » Polisi wateketeza madawa ya kulevya magunia 18 ya bangi na heroin



Na Mohab Dominick
0ct 28.2013
   Kahama


Jeshi la polisi wilayani kahama mkoani shinyanga ilimeteketeza jumla ya  madawa ya kulevya mbalimbali ya aina heroni,mirungi ,na bangi  madawa haya yalikamatwa maeneo tofauti katika wilaya ya kahama kwa kipindi cha January 2013 kwa mwaka huu.

Akisoma taarifa hiyo kaimu mkuu wa polisi wilayani kahama Elis haway (Asp)kwa kiongozi wa mbio za mwenge mwaka huu juma simai.alisema  jumla ya kesi za madawa ya kulevya zimekamatwa eneo la halmashauri ya mjini ni 17,watumiwa 62 walikamatwa ,na kesi 15 zimefikishwa mahakamani.

Adha  haway akifafanua zaidi alisema kuwa kesi 9,zimefanikiwa na kesi 6,zipo mahakamani zinaendelea mahakamani na kesi 2,zinaendelea na upelelezi.

Akifafanua zaidi mkuu huyo wa polisi kuwa katika halmashauri za msalala na ushetu  ambazo kipolisi  zinahudumiwa na polisi wilaya ya kahama zinaendesha msako katika maeneo yao na kupambana na madawa ya kulevya ,jumla ya kesi 10,zimelipotiwa katika vituo vya polisi vilivyopo katika halmashauri  ya kahama  na jumla ya watumiwa 19,walikamatwa,na kesi 8 zimefikishwa mahakamani na kesi 5 zimepata mafanikio na kesi 3zipo mahakamani  na kesi 2 zipo chini ya upelelezi.

Aidha  kaimu mkuu wa polisi Elis Haway alisema kuwa juhundi hizi zote zimetokana na mafanikio na mwitikio wa wanachi katika utoaji wa taarifa za waharifu wa madawa ya kulevya na kuwezesha kukamatwa kwao.

Naye kiongozi wa mbio za mwenge wa uhuru mwaka huu alisema kuwa kwa sasa ongezeni juhudi zaidi ziendelea kwa kushirikiana na wadau mbali mbali  kufanya misako ya pamoja na wilaya jirana na wanachi walio wema kwa hili na kuendelea kutoa elimu kwa wananchi  na hasa vijana  kuhusu madawa ya kulevya na kuokoa taifa letu kuwa na vijana walio adhirika na madawa haya.

mwisho
 

«
Next
Newer Post
»
Previous
Older Post

No comments:

Leave a Reply