sponsor

sponsor

Slider

Theme images by kelvinjay. Powered by Blogger.

Kimataifa Habari

habari

Habari Za Mastaa

Michezo

simulizi za kusisimua

» »Unlabelled » KESI YA ALBINO ALIYEKATWA MKONO YASHINDWA KUSIKILIZWA KAHAMA



Na  Mohab Dominick
Kahama
Oct 22, 2013.


MAHAKAMA kuu kanda ya Tabora iliyoketi Wilayani Kahama Mkoani shinyanga juzi ilihairisha shauri namba 2/2012 la kosa la jinai ililokuwa likiwakabili washitakiwa watatu la kosa shambulio la hatari lenye kusababisha ulemavu wa kudumu kwa Kabula Nkalango (albino).

Kesi hiyo ambyo ilikuwa imepngwa kusikilizwa juzi kwa mara ya kwanza  na Jaji Sam Rumanyika kutoka Mahakama Kuu Tabora  inawakabili washitakiwa Magobo Njige, Bupina Mihayo pamoja na Senga Mabirika.

Jaji Rumanyika alichukua  maamuzi ya kuhairisha kesi hiyo baada ya uapnde wa Washitakiwa kuwa na wakili mmoja ambaye ni John Ng’wigulila badala ya kila mshitakiwa kuwa na wakili wake wa utetezi Mahakamani hapo.

Washitakiwa wote watatu wanathumiwa kwa kosa la hatari kwa Mlemavu Kabula Nkalango Mlemavu wa ngozi (Albino) lililotendeka katika kijiji cha Luhaga Wilayani Kahama mkoani shinyanga mwaka 2012.

Kushindikana kusikilizwa kwa mara ya kwanza kwa kei hiyo ya jinai  kulidhaniwa kuwa wakili mmoja angetosha kuwatetea washitakiwa hao lakini mambo yalienda tofauti kwa watuhumiwa kutoelewana hali ambayo ilifanya mahakama hiyo isiweze kuoendelea hadi wote watatu watakapopatikana.

Kutokana na sababu hiyo Jaji Sam Rumanyika alililazimika kuhairisha kesi hiyo hadi tarehe 13/11/ 2013 ambapo kila mshitakiwa katika kesi hiyo atakuwa na wakili wake kwa ajili ya utetezi pamoja na mashahidi.

Mwisho.

«
Next
Newer Post
»
Previous
Older Post

No comments:

Leave a Reply