sponsor

sponsor

Slider

Theme images by kelvinjay. Powered by Blogger.

Kimataifa Habari

habari

Habari Za Mastaa

Michezo

simulizi za kusisimua

» »Unlabelled » WENYE USHAHIDI WA KULIWA NGO’MBE ZAO SERIKALI HAITASITA KUWACHUKULIA HATUA WAHUSIKA; JKNa  Mohab Dominick
Geita
Nov 11, 2013.
 Rais jakaya mrisho kikwete Akihutubia wakazi wa uyovu wilayani Bukombe katika unziduzi wa barabara ya uyovu Bwanga yenye urefu wa kilometa 45 kwa kiwango cha lami picha na mohab Dominick.


Rais wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania Jakaya Mrisho Kikwete amesema kuwa kama kuna mtu jamii ya wafugaji ambaye ng’ombe zake zimepigwa Risasi na Askari wa wanyamapori katika operesheni serikali kali haitasita kuwachulia hatua wahusika.

Rais Kikwete aliyasema hayo wakati akiwahutubia wakazi wa Mji wa Ushirimbo katika mkutano wa hadhara juzi wakati wa ziara yake inayoendelea ya kukagua shughuli mbalimbali za maendeleo katika Mkoa wa Geita.

Alisema kuwa kwa sasa Kiwango cha uwindaji wa wanyapori kimefikia kiwango cha kutisha hali ambyo Serikali haiwezi kuvumia uharamia huo na kuongeza kuwa katika hifadhi sio mahali pa kulishia Ng’ombe bali na mahali pa kulishia wanyama pori.

“Nasema kama kuna mfugaji ambaye ng’ombe zake zimepigwa Risasi na Askari wetu wa Wanayamapori na ana ushahdi na uhakika wa kufanyika kwa vitendo hivyo basi Serikali haitasita kuwachulia hatua Askari waliohusika”, Alisema Rais Kikwete.

Pamoja na Mambo mengine katika hutuba yake hiyo Rais Kikwete alitoa tahadhari juu ya ongezeko la maambukizo ya Ugonjwa hatari wa Ukimwi katika Wilaya ya Bukombe kwani hadi kufikia sasa maambukizo hayo katika Wilaya hiyo yamefikia asilimia 6.3  kuzidi ile ya kitaifa ambayo ni 5.1.

Aidha aliendelea kusema kuwa jumla ya watu 8,100 katika Wilaya hiyo wanaishi na Virusi vya ukimwi  huku watu 5,100 ndio wanaotumia vidonge vya kurefusha maisha (ARV) na kuongeza kuwa sehemu zinazoongoza kwa maambukizo ni pamoja na sehemu zenye machimbo madogomadogo.

Alizitaja sehemu hizo kuwa ni pamoja na Katente, Kerezia pamoja na uyovu na kuongeza kuwa watu hawana budi kubadilika na kuwasikiliza mawaidha kutoka kwa viongozi wa dini juu ya tahadhari ya ugonjwa huo ambao umekuwa tishio hapo nchini.

Hata hivyo alisema kuwa ili kupunguza maambukizi ya ugonjwa huo lazima watu wabadilike na kuwa waaminifu kwa wapenzi wao ikiwa ni sambamba na kutumia kinga wakati wa kufanya kitendo hicho.

mwisho

«
Next
Newer Post
»
Previous
Older Post

No comments:

Leave a Reply