sponsor

sponsor

Slider

Theme images by kelvinjay. Powered by Blogger.

Kimataifa Habari

habari

Habari Za Mastaa

Michezo

simulizi za kusisimua

» »Unlabelled » BUZWAGI YAUPONGEZA UONGOZI WA SHULE YA SEKONDARI MWENDAKULIMA KUCHUKUA NAFASI YA KWANZA KADA YA ZIWA


mwalim mkuu wa shule ya mwendakulima Diana kuboja akiwa ofisini kwake kabla ugeni kutoka African barrick Gold mine kuwasili shuleni hapo

 haya ndiyo maneno mkuu wa shule karibuni aliye na gauni jekundu ni mkuu wa shule ya mwendakulima Diana kuboja kwa mtendaji wa kata cisilia wakati walipowasili shule hapo .
 karibu mkuu wa shule ya mwendakuli Diana kuboja akimkaribisha makamu wa Rais wa African barrick Gold mine Deo mnyika shule hapo karibu .
 karibuni sana wageni wetu
 karibu shule wageni mwenye gauni jekundu ni afisa mahusiano wa barrick blandina mughezi wakiwasili shule hapo .
 kushoto ni afisa mahusiano wa barrick blandina mughezi kati ni mkuu wa shule ya mwendakuli Diana kuboja na kulia ni makamu wa Rais wa (ABG )Deo mnyika shuleni hapo.
 Meneja wa Mgodi wa Buzwagi Filber Rwenyemamu.akitoa neno kwa wageni walikwa.
 Makamu wa Rais Deo Mnyika akitoa pongezi kwa uongozi wa shule kwa kufanya vizuri katika mithiani yao ya kidato cha sita mwaka jana .

 Assa Mwaipopo meneja mahusiano wa (ABG )akiwapongezi walimu na wanafunzi kwa kuipa shule hiyo heshima kubwa kwa kufanya vizuri na kushika na nafasi ya kwanza kwa kanda ya ziwa kwa shule za kata .
 Baadhi ya wanafunzi wa shule ya sekondali ya mwendakulima wakiwa katika ukumbi wao wa mkutano na uongozi wa African barrick gold mine.
 Pokea zawadi ya ngao na medal ya kufanya vizuri na kuipa heshima mgodi wa Buzwagi mwenye tai ni ass mwaipopo.
 Asanteni sana hii zawadi kwa shule yetu.
 Asante
pokea zawadi ya kufanya vizuri
Rais wa African barrick Gold mine Deo mnyika akimbidhi zawadi walimu mkuu wa shule ya mwendakuli ngao.
Asante sana kwa heshima hii .
meneja wa mgodi wa buzwagi Filber Rwenyemamu akishukuru mkuu wa shule Diana kuboja .
Afisa mahusiano wa barrick blandina mughezi akimukabidhi ua kama ishara ya upendo kati ya mgodi na shule hiyo .
picha ya pamoja
Asante mwalimu
mwalimu Diana kuboja akipokea msaanda wa madaftali ya kuandikia toka kwa Rais wa African barrick Gold mine Deo mnyika shule hapo.
pokea mwalimu madaftali na vitabu vyenye samani ya milioni 10.2
pokea ngao ya heshima toka uongozi wa Africa barrick gold mine

picha yapamoja na uongozi wa shule .

ukanguzi wa shule mbele mwenye sharti njeupe ni makamu wa rais wa Africa barrick gold mine Deo mnyika.

Makamu wa Rais Deo mnyika akiongea na baadhi ya wanafuzi wa shule ya mwendakulima wakati wa ziara yake ya kupongeza shule hiyo kwa kufanya vizuri katika mithiani yao ya kidato cha sita.
Deo mnyika mwenye shati jeupe akipata maelezo juu ya mwili wa binadamu uliyo toka kwa mwanafuzi wa kidato cha kwanza.
hapa ndipo kwenye huduma ya kwanza karibuni .
 

KAMPUNI  ya African Barrick Gold. Kupitia Mgodi wake wa Dhahabu Buzwagi ABG umeupongeza uongozi wa shule ya Sekondari  Mwendakulima kutokana na kufanya vizuri  katika mitihani wa Taifa kidato cha sita 2013 na kuchukua nafasi ya kwanza kanda ya Ziwa.
Pongezi hizo zimetolewa leo na Meneja wa Mgodi huo,Filbert Rweyemamu wakati wa tafrija fupi ya kuupongeza uongozi wa Shule hiyo iliyofanyika shuleni hapo sambamba na kukagua miradi mbalimbali iliyotolewa na mgodi huo.

Katika hatua ya pongezi hizo Meneja huyo amemsifu mkuu wa shule hiyo na kuwaeleza umati uliohudhulia Tafrija hiyo  kuwa mkuu huyo wa shule amekuwa ni nguzo kubwa katika mafanikio makubwa kwa kuushirikisha uongozi wa mgodi huo.

Aidha Rweyemamu amesema kuwa mgodi umekuwa mstari wa mbele kuhakikisha Shule hiyo inaboreshwa kwa kiwango kilicho cha hali ya juu kuahidi iwe mfano bora kwa shule za sekondari za kata kutokana shule hiyo ipo jirani zaidi na Mgodi huo.

Rweyemamu amefurahishwa na kitendo cha watoto wa kidato cha sita katika shule hiyo kujituma vilivyo katika mtihani wa taifa wa mwaka jana  ambapo amesema kati ya shule 180 za kanda yaZiwa Mwendakulima ilichukua nafasi ya kwanza.


Hata hivyo amewataka wanafunzi kuichukua fursa hiyo na kuigeuza kuwa changamoto kwao wasibweteke na kujisifu badala yake waongeze bidii ili mitihani ijayo waweze kufanya vizuri ngazi ya kitaifa na siyo kanda ya ziwa na kuwaahidi kuwa mgodi utawashika mkono kwa hali na mali.

Kwa upande wake Afisa elimu sekondari wa Halmashauri ya mji wa Kahama,Richard james Sadati akimwakilisha mkurugenzi wa mji huo,Felix Kimaryo ameushukuru mgodi huo kwa kuipa kipaumbelele Shule hiyo hali iliyo sababisha matokeo mazuri katika shule hiyo nakuuomba mgodi uzidi kujitolea katika Nyanja za elimu katika mji huo. 

Hata hivyo mkuu wa shule hiyo,bi. Diana Kuboja, amesema mgodi umesababisha shule hiyo kuleta heshima kwa shule za kata kutokana na kuvunja rekodi  kwa  kufanya vizuri, na kuyaomba mashirika mengine nayo yajikite katika kuzishika mkono shule za kata ili kukuza kiwango cha elimu kwa shule za kata. 

Katika hatua nyingingine meneja wa mgodi huo,Rweyemamu amesema mgodi wake unasomesha watoto 200 wanaoishi katika  mazingira magumu ambapo katika pongezi hiyo mgodi huo umetoa zawadi kwa shule hiyo pamoja na vifaa vya masomo vyenye thamani ya shilingi m.10.2

Mwisho.


«
Next
Newer Post
»
Previous
Older Post

No comments:

Leave a Reply