sponsor

sponsor

Slider

Theme images by kelvinjay. Powered by Blogger.

Kimataifa Habari

habari

Habari Za Mastaa

Michezo

simulizi za kusisimua

» »Unlabelled » mashindano ya mbio za baiskeli yafana kahama

Mgeni rasmi naibu waziri wa utamaduni na michezo Juma Nkamia Akihutubia maelfu ya wakazi wa mji wa kahama kwenye mashindano ya mbio za baiskeli ambayo yamefadhiliwa na Mgodi wa African barrick Gold mine Buzwagi
Mbuge wa kahama jemes lembeli akitoa salamu kwa wakimbiza baiskeli kabla hajamkaribisha mgeni rasim Naibu waziri utamaduni na michezo Juma Nkamia  .

Baadhi ya umati mkubwa uliojitokeza kuona mashindano ya mbio za baiskeli katika uwanja wa taifa kahama .

Mshindi wa pili toka shinyanga akibidhiwa kikombe na mkuu wa wilaya ya kahama Benson Mpesya
Mshindi wa tatu toka mwanza mbio za Baiskel akipokea fedha tasilmu laki saba  toka kwa meneja wa mgodi wa Buzwagi Filber Rweyemamu .
Mkuu wa wilaya ya kahama Benson mpesya akimpokeza mshindi wa tatu toka musoma na nyuma yake ni meneja wa mgodi wa Buzwagi Filber Rweyemamu mwenye kofia nyuma ya mkuu wa wilaya ya kahama


Mshindi wa kwanza kwa mwanawake Matha Anthony ambaye alikibia kilometa 80 toka kahama hadi kijiji cha sungamile ambapo alipata fedha taslmu milioni moja .
Mshindi wa pili Seni konda toka shinyanga alinye na bahasha akibidhiwa na Naibu waziri wa utamaduni na michezo Juma Nkami wa kati ana alishika medal ni makamu wa Rais wa African Barrick Gold mine.
Mshindi wa kwanza wa mbio za baiskeli masunga Duba ambaye alikimbia kilometa 156.5 toka kahama hadi tinde kwenda na kurudi ambapo alijinyakulia fedha taslmu milioni moja na nusu
 mkuu wa wilaya ya kahama Benson mpesya akimbidhi mshindi wa mbio za baiskeli kwa mwanawake za kilometa 80 matha Athony  kujinyakulia milioni moja.
picha ya pamoja naibu waziri wa utamaduni na michezo juma Nkamia mwenye kofia mbele ya mshindi wa pili mwenye bahasha mkononi seni konda ambaye alinyakulia kitita cha milioni moja .
mshindi wa pili wa mbio za Baiskeli Seni konda akinua mikono juu baada ya kukabidhiwa kikombe na fedha milioni anaye piga makofi ni makamu wa Rais wa( ABG)Deo mnyika katika viwanja vya halmashauri ya kahama (Marufu uwanja wa Taifa )
Na Mohab Dominick
    August 2014
    
Mashindano ya mbio za baskel wilayani kahama mkoani shinyanga yazidi kutimuwa vumbi katika viunga mbalimbali wilyani humo yaliyodhaminiwa na Kampuni ya uchimbaji wa Madini African Barick Gold.Kupitia mgodi wa dhahabu Buzwagi ABG wakishirikiana na chama cha waendesha Baiskel Tanzania.

Mashindano hayo yaliyokuwa pata shika nguo kuchanika kutafuta mshingi wa kwanza hadi wa ishirini kwa wavulana pamoja na wasichana ambapo yalikutanisha mikoa 6 ya kanda ya ziwa  ambayo ni Mara, Mwanza , Geita,Kagera, Simiyu pamoja na shinyanga.

Katika mbio hizo za baiskeli zilizowakutanisha washiriki wa jinsia zote huku wavulana wakikimbia kilometa 156.5 kutoka maeneo ya faphtom kuelekea manzeshe hadi shinyanga vijijini ambapo wasichana wakikimbia kilometa 80 kutoka maeneo ya faphtom kuelekea manzese hadi Sungamile Isaka,huku wote kumalizia mashindano hayo katika  barabara ya Bijampola mjini kahama.

Kwa upande wake katibu Mkuu Taifa chama cha waendasha  baiskeli John Machemba awali akizungumza katika ufunguzi wa mbio hizo wilayani humo amesema kuwa lengo la mashindano hayo ni kutafuta washindi 20 kutoka pande zote mbili kwa wanaume pamoja na wanawake ili kwenda kushiriki katika shindano lililoandaliwa huko mbeya litakalo shirikisha kanda 6.
Machemba alimtanganza  mshindi wa kwanza  kuwa Masunga Duba kutoka mwanza aliyekimbia masaa 4 na sekunde 3 huku akipata zawadi ya shillingi million 1.5, Medali pamoja na kikombe huku mshindi wa pili akitajwa kuwa ni Seni Konda kutoka shinyanga huku akipatia Tsh.million 1 na Medali pamoja na Kikombe.Pamoja na mshindi wa 3 Simon Mbaluku kutoka simiyu akipatiwa Tsh,laki 7.

Huku Mshindi wa 4 hadi wa 10 walipatiwa Tsh.laki 2.5 pamoja na wengine waliobaki ambao hawakuingia katika kumi bola walipatiwa Tsh,laki 1.5 ili kuwahamasisha kushiriki katika mashindano mengine kwa mwaka ujao.
Kwaupande wake Makamu wa Rais wa Kampuni ya uchimbaji Madini African Barick Gold.Kupitia mgodi wa dhahabu Buzwagi ABG,,Deo Mwanyika amesema kuwa kampuni hiyo inawajali wananchi huku lengo lake ikiwa ni kukuza vipaji mbalimbali ya vijana huku akiwataka kutumia fursa hiyo ili kutambua uwepo wawawekezaji katika maeneo yao

Nae naibu waziri wa habari,utamaduni vijana na michezo Juma Nkamia ameitaka  halmashauri ya mji wa kahama kutumia fursa hiyo ya wawekezaji kukuza vipaji mbalimbali ya vijana ikiwa ni pamoja na kubolesha mazingira ya michezo hususani uwanja  wa michezo wa halmashauri hiyo.

Pia ameutaka uongozi wa mgodi huo kushirikiana na ofisi yake katika kuulekebisha uwanja wa michezo wa halmashauri hiyo huku mgodi ukibolesha uzio(UKUTA) na ofisi yake ikipandikiza majani ya bandia pamoja na kubolesha mazingira ndani ya uwanja huo.

mwisho

«
Next
Newer Post
»
Previous
Older Post

No comments:

Leave a Reply