sponsor

sponsor

Slider

Theme images by kelvinjay. Powered by Blogger.

Kimataifa Habari

habari

Habari Za Mastaa

Michezo

simulizi za kusisimua

» » » WACHIMBAJI WADOGO KAHAMA WAPATA NEEMA YA MAENEO YA UCHIMBAJI.

 Mkuu wa wilaya ya kahama Benson Mpesya ambaye pia ni mwenyekiti wa kamati ya kungawa viwanja vya uchimbaji mdogo wilayani kahama .
 Baadhi ya wajumbe wa kamati ya ugawaji wa viwanja vya wachimbaji wadogo katika machimbo ya nyangalata na mwime  wilayani kahama
 Mwenyekiti wa kamati ya ugawaji wa viwanja vya wachimbaji wadogo ambaye pia ni mkuu wa wilaya ya kahama Benson mpesya akiongea na waadishi wa habari juu ya makapuni makubwa ya uchimbaji yalivyotoa maeneo yao kwa ajili ya wachimbaji wandogo.
 Afisa madini wa wilaya kahama sophia mwenye miwa kati akiwa kati ya wajumbe wa kamati hiyo
 Mwenyekiti wa kamati ya ugawaji wa viwanja vya wachimbaji wadogo pia ni mkuu wa wilaya ya kahama akifafanua jambo kwa waandishi wa habari hawapo pichani .
 Baadhi ya wajumbe wa kamati ya ugawaji wa viwanja vya wachimbaji wadogo katika machimbo ya nyangalata na mwime wilayani kahama .
Mkurungezi wa Halimashauri ya msalala patrick charles akiwa moja wa wajumbe wa kamati ya ugawaji wa viwanja vya wachimbaji wadogo katika machimbo ya nyangalata na mwime .

Na  Mohab Dominick
Kahama
Agust 1, 2014.

HATIMAYE  Serikali kupitia Wizara ya Madini na Nishati imeanza kusikiliza kilio cha Wachimbaji wadogowadogo kuhusu maeneo ya uchimbaji baada ya kuinyanganya Kampuni ya  African Barrick Gold na Pangea Mineral baadhi ya maeneo waliokuwa yanaleseni za Kampuni hizo na hawayatumii kisha kuwamilikisha wachimbaji wadogowadogo.

Mkuu wa Wilaya ya Kahama Benson Mpesya aliyasema hayo juzi wakati akizungumza na Waandishi wa Habari kuhusu nia ya Serikali kuanza kutatua matatizo ya Wachimbaji wadowadogo kuhusu maeneo yalikuwa na leseni za wachimbaji wakubwa na kutoyafanyia shughuli za uchimbaji.

Mpesya alisema kuwa baadhi ya maeneo waliopewa wachimbaji wadogo ni pamoja na eneo la Nyangalata ambaolo lilikuwa na leseni Kampuni ya African Barrick Gold na eneo la Mwime ambalo lilikuwa likimilikiwa na Kampuni ya Pangea Mineral.

Mkuu huyo wa Wilaya akiwa na Kamati ya watu saba ya ugawaji wa Viwanja vya madini alisema kuwa Serikali ilitangaza kuwa itatoa nafasi kwa wachimbaji wadogowadogo ambao kwa kaisi kikubwa wamekuwa wakivamia na kuongeza kuwa katika maeneo ya Nyangalata na Mwime  leseni ya Barrick imefutwa na kupewa wachimbaji wadogowadogo.

Aidha aliendelea kusema kuwa maeneo hayo kwa sasa hayana leseni na kuongeza kuwa ugawaji wa maeneo hayo utaangaliwa upya na kuongeza kuwa kwa watu wanaotaka maeneo kwa sasa hawanabudi kuomba upya leseni za kumiliki na hiyo ni kwa mujibu wa kamati ya ugawaji wa viwanja vya madini ilivyopanga.

Aidha Mkuu huyo wa Wilaya alisema kuwa maombi ya kuomba yataanza kupokelewa kuanzia tarehe 2/8/2014 hadi kufikia tarehe 31/8/2014 na kuongeza kuwa anayetaka maeneo hayo nafasi ipo wazi lakini kwa sasa maeneo hayo ni mali ya wachimbaji wadogowadogo wa maeneo hayo.

Pia aliwataka wachimbaji wadowadogo kuhakikisha kuwa wanaunda ushirika na kuusajili na kungeza kuwa serikali inataka kuona rasilimali hiyo ya dhahabu inanufaisha watanzanzania kuanzia katika ngazi ya vijiji na Taifa kwa ujumla na kuhakikisha kuwa Wilaya ya Kahama inapata mgodi wa tatu utakaotokana na wavchimbaji hao wadogo.

Kwa upande wake Kamishna msaidizi wa Madini Kanda Hamphrey Mmbando alisema kuwa kutokana na Serikali kuwakumbuka wachimbaji wadogo ni suala la msingi kwani hapo awali walikuwa wakihangaika kuvamia maeneo yenye leseni za Wachimbaji wakubwa au watafiti.

Alisema kuwa katika eneo la Mwabomba bado mazungumzo yanaendelea vizuri baina mtafiti amayefanya kazi hapo ambaye ni Kampuni ya Rift Valley Resouses na Kamati hiyo na kuongeza kuwa kama kutakuwa na makubaliano mazuri basin a eneo hilo wanaweza kupewa wachimbaji hao wadogo.

Mwisho.

«
Next
Newer Post
»
Previous
Older Post

No comments:

Leave a Reply