sponsor

sponsor

Slider

Theme images by kelvinjay. Powered by Blogger.

Kimataifa Habari

habari

Habari Za Mastaa

Michezo

simulizi za kusisimua

» » DC.MARUFUKU KUFANYA MIKUTANO YA HADHARA HALMASHAURI YA MSALALA

 Baadhi ya mikutano mikubwa kama hii imepingwa marufuku jimbo la msalala katika halmashauri ya msalala wilayani kahama .


 Umati wa wananchi wakiwa katika mikutano ya kawaida ya hadhara ambapo mkuu wa wilaya ya kahama benson mpesya kwa sababu ya kisiasa wilayani kahama .


Na Mohab Dominick
   kahama
  Sept 2,2014
DC MARUFUKU KUFANYA MIKUTANO YA HADHARA HALMASHAURI YA MSALALA .

SERIKALI  wilayani Kahama kupitia kamati yake ya Ulinzi na Usalama ya wilaya imepiga marufuku kufanyika kwa mikutano,maandamano pamoja na sherehe kwa wananchi wote wa Halmashauri mpya ya Msalala baada ya kubaini kuwepo kwa uvunjaji wa amani.

Hali hiyo imetangazwa jana na Mwenyekiti wa kamati ya ulinzi na Usalama  ya wilaya ya Kahama Benson Mpesya baada ya kubaini kuwepo kwa mikutano,maandamano pamoja na sherehe baada ya Waziri Mkuu;Mizengo Pinda kutangaza Makao MaKuu ya Halmashauri hiyo Busangi.

Wananchi hao kupitia madiwani wao walikuwa na Mgogoro wa siku nyingi wa kugombea Makao Makuu hayo,ambapo awali wakati wa kuanzishwa kwa halmashauri hiyo ya  Msalala,serikali ilitangaza makao makuu hayo kuwa kata ya Busangi.

Hata hivyo baada ya muda baadhi ya Madiwani walibadirisha Makao Makuu hayo kwa kuyahamishia Kata ya Segese hali ambayo ilizua mvutano mkubwa wa kugombea ujenzi huo hali ambayo Waziri Mkuu aliingilia kati kupinga kuhamishwa kwa Makao hayo.

Kufuatia hali hiyo mwishoni mwa wiki iliyopita wananchi wa Msalala waligawanyika kwenye makundi mawili ambapo wengine waliunga mkono uamuzi wa Waziri Mkuu kwa sherehe huku wengine wakipinga  kwa maandamano na mikutano.

Hali hiyo kwa mujibu wa Mwenyekiti huyo ambaye pia ni Mkuu ya wilaya ya Kahama amesema ili kulinda amani kwa wananchi Serikali imepiga marufuku mikutano ama mikusanyiko ya aina yoyote mpaka pale watakapotangaziwa.

Mwisho

«
Next
Newer Post
»
Previous
Older Post

No comments:

Leave a Reply