sponsor

sponsor

Slider

Theme images by kelvinjay. Powered by Blogger.

Kimataifa Habari

habari

Habari Za Mastaa

Michezo

simulizi za kusisimua

» » MAUAJI YA VIKONGWE KAHAMA



Na Mohab Dominick
Sept 2 ,2014
Kahama
Mtu moja Auwawa kikatili kahama kwa imani za kishirikina.

WAKATI Serikali wilayani Kahama,ikiwa katika mikakati ya kukomesha mauaji ya vikongwe kwa kuwatambua kwa kuwapigia kura wauaji wa kukata mapanga,tayari janga hilo limeingia mjini baada y mtu mmoja juzi kuuawa kwa kukatwa mapanga kilometa chache kutoka katikati ya Mji wa Kahama.

Tukio hilo limetokea katika mtaa wa Ilindi katika Halmashauri ya mji wa Kahama,baada ya wauaji hao kumuua kwa kumkata mapanga Elias Hungwi {52} mkazi wa Kata ya Zongomera ambapo  watu hao wanaokadiriwa kuwa sita walivunja mlango wa nyumba yake kwa kutumia jina la Fatuma.

Kwa Mujibu wa Afisa Mtendaji wa Kata hiyo,Ally matisho watu hao baada ya kuingia ndani waliingia chumba alichokuwa amelala Hungwi pekee yake baada ya mkewe,Yasinta Lugaranzura kumuacha chumbani kwake  alale na wageni wa kike waliokuwa wamewatembelea.

Matisho amesema baada ya kufika humo ndani walianza kuomba wapewe Shiringi Milioni Mbili wakidai Marehemu Hungwi alizipata fedha hizo baada ya kuozesha binti yake miezi miwili iliyopita baada ya kuzikosa walimuua kwa kumkata mapanga.

Hata hivyo Hungwi miezi miwili iliyopita amemuozesha Mtoto wake wa Kike kwa kiasi cha Shilingi Laki Sita lakini wauaji hao waliomba kupewa Shilingi Milioni Mbili ambazo hazikuwepo kwenye familia hiyo.Mwisho

Jeshi la Polisi kupitia Kamanda wake wa  Mkoa wa Shinyanga;Justus Kamugisha  linawashikilia watu watano wana familia hiyo,wakiwemo wageni waliofika hapo na kulala chumba cha Marehemu huyo na mkewe hali iliyofanya alale chumba kingine mpaka alipopatwa na mauti hayo.

Aidha kamanda  wa jeshi la   polisi mkoa wa shinyanga Justus kamugisha  amewataka wananchi kutoa taarifa kwa vyombo husika ili tuweze kuwa kamata watu wanaonyanfa  mauji hayo na kulipa jeshi la polisi hushirikiano wa pamoja.kwa kutomeza mauwaji hayo.

 Mwisho

  

«
Next
Newer Post
»
Previous
Older Post

No comments:

Leave a Reply