sponsor

sponsor

Slider

Theme images by kelvinjay. Powered by Blogger.

Kimataifa Habari

habari

Habari Za Mastaa

Michezo

simulizi za kusisimua

» » » MAUAJI YA ASKARI POLISI YATOLEWA NA IGP MANGU

IGP  Ernest mangu akitoa salamu za mwisho kwa askari polisi aliyeuwa .
Kamanda wa Polisi Mkoa wa Dodoma, David Misime (SACP) amefafanua kuhusu kilichomsibu mtuhumiwa wa mauaji ya askari polisi Joseph Isack Swai.

Kamanda huyo alisema kwamba baada ya mauaji ya askari huyo, wananchi walikusanyika na kuanza kumsaka mtuhumiwa Tissi Siril malya na majira ya saa tano usiku walimkuta maeneo ya Mti Mkavu maili mbili mkoani Dodoma.

Alisema kwamba wananchi walimkuta mtuhumiwa na panga alilotumia kumuua askari na kuanza kumshambulia.

Pamoja na Polisi kuwahi kufika eneo la tukio na kumchukua kumkimbiza Hospitali ya Mkoa lakini daktari akagundua ameshafariki. 

Aidha Kamanda Misemi amesema mtuhumiwa huyo katika kumbukumbu tulizonazo ni kwamba mwaka 2006 aliwahi kufungwa miaka mitatu (3) kwa kosa la kujeruhi, Pia mwaka 2009 alifungwa tena miezi sita (6) kwa kosa la kutishia kuua. 

Aidha pamoja na kutoa pongezi kwa wananchi kwa kuonyesha kuchukizwa na kitendo alichomtendea Askari ,lakini amewataka kuacha kujichukulia sheria mkononi.

Pia ametoa wito kwa wananchi tuanze kuchukua hatua kurekebisha maadili kuanzia ngazi ya familia kwani tumeelezwa kuwa mtuhumiwa alikuwa ni mvutaji bangi kiasi kwamba ilimfanya awe anafanya vitendo ambavyo ni kinyume na maadili na sheria za nchi.

Wakati huo huo  Mkuu wa Jeshi la Polisi nchini (IGP), Ernest Mangu aliongoza mamia ya wakazi wa Dodoma kumuaga Askapo Polisi aliyeuawa wakati akitekeleza majukumu yake na  na kuliagiza Jeshi la polisi kuongeza kasi ya kupambanana uhalifu na wahalifu.

Askari huyo aliyeuawa Koplo Joseph Swai (27) tayari amesafirishwa kwendaArusha kwa mazishi.

IGP Mangu alisema Jeshi la polisi linatakiwa kuongeza kasi ya kupambana nauhalifu kutokana na kuongezeka kwa vitendo hivyo ndani ya jamii.

“Kijana amekufa kishujaa wakati akitetea mtu asiye na uwezo wakatiakinyanyaswa, katika kifo hiki askari wapate cha kujifunza kwani kimewatianguvu na kuwawezesha kufahamu namna ya kukabiliana na uhalifu.

Alisema msiba huo ni fursa ya kujihami na kukomesha uhalifu.
Naye Mkuu wa Mkoa wa Dodoma. Chiku Gallawa alisema ni wajibu wa jamiikufichua wahalifu ili waweze kukabiliana na mikono ya sheria.

Mbunge wa viti maalum Moza Abeid aliitaka jamii  kufichua waovu kwani wako kwenye familia na wanajulikana na iwapo wangekuwa wakitajwa ni vizuri kuliko kuachwa mpaka wanapoleta madhara makubwa kwa jamii.

Akimwakilisha kamanda wa polisi Mkoa wa Dodoma, kamishna msaidizi wa Polisi, Emmanuel Lukula alizitaka familia kulea watoto wao katika njia ya kukataa uhalifu.

 Mwisho

«
Next
Newer Post
»
Previous
Older Post

No comments:

Leave a Reply