Naibu Kamishina wa Uhamiaji Mkoani shinyanga Anamaria Yondani.
Baadhi ya baiskeli zinazotumika kwa wahamiaji haramu
ambapo idara ya uhamiaji mkoa wa shinyanga wamefanya msako mkali na
kukamata waendesha bodaboda wa baiskeri na kujifanya ni wakazi wa wilaya
ya kahama mkoani shinyanga,
Baiskeli ambazo zimekamatwa na idara ya uhamiaji wilayani kahama
Idara
ya uhamiaji wilayani Kahama Mkoani Shinyanga imewakamata Raia 12 kutoka nchi
jirani ya Burundi kwa kosa la kuingia, kuishi na kuendesha shughuli mbali
mbali hapa Nchini bila vibali jambo
ambalo ni kinyume cha Sheria za nchi.
Kukamatwa
kwa watu hao kumefuatia Operesheni maalum ya Idara hiyo ngazi ya Mkoa
ikiongozwa na Naibu Kamishina wa Uhamiaji Mkoani humo Anamaria Yondani.
Naibu
kamishina huyo alisema msako mkali kwakutumia mbinu mbali mbali za jeshi la uhamiaji
ndio uliopelekea kuwakamata raia 10 wakiendelea na shughuli zao katika maeneo
mbali mbali ya Mji wa kahama ambapo wawili walijisalimisha wenyewe katika ofisi
za uhamiaji.
No comments: