KAHAMA
Chama cha Demokrasia na maendeleo CHADEMA wilayani Kahama Mkoani
Shinyanga Kimetoa tamko la Kuiomba Serikali kurejesha Msaada wa mabati zaidi ya
800 yaliyotolewa na Chama hicho kwaajili ya ujenzi wa Nyumba za wahanga wa
Mafuriko
Tamko la Chama hicho kudai msaada huo limetolewa na Mwenyekiti
wa Chama hicho Juma Protase Ntaimpera ambaye alisema azimio la Chama hicho
linatokana na Tamko la Rais John Magufuli kubainisha kuwa Serikali haina nia ya
kujenga nyumba za wahanga hao
Ntaimpera alisema kutokana na tamko hilo la Rais alilotoa wakati wa ziara yake Wilayani Kahama mwshoni
mwa mwezi julai mwaka huu,CHADEMA waliandika barua kwa Mkuu wa Wilaya
kuitaka Serikali kurejesha msaada huo
Mwenyekiti huyo,alisema baada ya serikali kurejesha Mabati hayo
Chama kitayagawa kwa watu wenye mahitaji ili wayatumie katika ujenzi kwakuwa
wanaishi katika mazingira magumu.
Ntahimpera aliongeza kuwa ,CHADEMA walitoa msaada huo kwa nia
njema kwaajili ya kuwasaidia wahanga wasiojiweza hasa kwakuzingatia umu wa
maisha wanaokutana nao baada ya Mvua kubwa iliyoambatana na Upepo mkali kuezua
nyumba zao ,baadhi ya wananchi wa Kijiji cha Mwakata kata ya Mwenda
ulimakubaki bila makazi na wengine kupoteza maisha
No comments: