Na Mohab Dominick
Kahama
Oct 28, 2013.
Mkuu wa shule ya Rocken Hill Alexander kazimiri akipongeza msichana kwa kuongoza masomo yote.
IMEELEZWA kuwa kwa wakati
huu Mwanafunzi akishindwa kusoma kwa bidii hakuna haja ya kumlalamikia mzazi
kwani wanapata kila kitu tofauti na waliopata Elimu katika kipindi cha nyuma.
Hayo yalisemwa juzi na
Mkuu wa Shule ya Sekondari ya Anderleck Adamu Rui katika sherehe za mahafali ya
tano ya shule hiyo yaliofanyika juzi mjini Kahama na kuongeza kuwa msingi
Mkubwa wa maisha ni elimu kwa sasa.
Rui alisema kuwa kwa
maisha sasa katika maisha ya sasa sio wanafunzi wote wanapenda shule na
kuongeza kuwa wengine ni wakuvumiliana sana kutokana na tabia walizonazo
mashuleni kwani wao ndio wanawajua kwa undani zaidi kwa kuwa wanaishi nao kila
siku tofauti na wazazi.
Alisema kuwa wanafunzi wa
sasa wanapatak kila kitu kutoka kwa wazazi wao tofauti na wale waliokuwa
wakisoma katika kipindi cha nyuma hali ambayo wao wanapaswa kuwa kioo cha
kwanza na mfano kwa wengine wanaoanza shule.
Aidha Mkuu huyo wa shule
aliendelea kusema kuwa suala kubwa kwa mwanafunzi kwa sasa ni mafanikio ya
mbeleni na sio kuangalia muda unaendaje bali ni kuangalia yeye kama Mwanafunzi
ameutumiaje muda alipokuwa shuleni ili aweze kupata mafanikio.
Kwa upande wake Mkurugenzi
wa Shule ya Anderleck Alexander Kazimiri alisema kuwa wazazi hawana budi
kushirikina na walimu katika kuwalea wanafunzi hasa katika masuala makubwa ya
maadili na malezi yalio mema hali ambayo italeta mafanikio katika mitihani yao.
Kazimiri alisema kuwa
katika maisha ya sasa Vijana wengi wamekuwa na tabia ya kulalamika tuu bila ya
kufanya kazi ikaonekana na kujua kuwa wazazi wapo nyuma yao katika kusimamia
malezi yao wanayoyapata tangu wakiwa shuleni hadi wanapomaliza.
“Unajua kwa sasa Vijana
wengi wana tabia ya kujua tamthilia za kwenye Runinga kuliko kusoma vitabu huku
ikichangiwa na kutokwenda katika maktaba mbalimbali kwa ajili kujikumbusha yale
waliokuwa wakifundishwa”, Alisema Alexander Kazimiri.
Kwa upande wake Mgeni
rasmi katika mahafali hayo yaliojumiuisha wanafunzi 152 Mkuu wa Polisi Mstaafu
George Simba aliwataka wanafunzi kudumisha nidhamu ambayo kwa sasa imeshuka kwa
kiwango kikubwa kwa wanafunzi.
Pia aliwataka wazazi
kuwasaidia vijana hao katika mambo mbalimbali hususani Elimu ili waweze kutimiza
ndoto zao walizojiwekea ikiwa ni sambamba na kudhibiti nidhamu wakati wowote
watakapokuwa nyumbani wakisubiri matokeo.
Mwisho.
No comments: