Na Mohab
Dominick
Kahama
04 nov , 2013.
mkuu wa wilaya ya kahama Benson mpesya akisisitiza jambo kwa watendaji wa vijiji na kata
MKUU wa Wilaya ya Kahama Benson Mpesya amewataka
Watendaji wa kata na Vijiji kuacha kuwachangisha wananchi michango mbalimbali
ya maendeleo katika kipindi cha kuanzia
mwezi wa kumi.
Aliyasema hayo wakati wa Kikao cha Maendeleo ya
Wilaya ya Kahama (DCC) na kuongeza kuwa katika kipindi hicho wananchi wanakuwa
katika kipindi cha kilimo na kuelekeza nguvu zao katika kupata chakula cha
kipindi kijacho.
Mpesya alisema kuwa kama Watendaji hao watawatoza
michango katika kipindi hicho Wakulima watakosa fedha za kulimia hali ambayo
inaweza kuleta upungufu wa chakula kwa kuwa nguvu zao watakuwa wameelekeza
katika michango.
Aidha Mkuu huyo wa Wilaya aliwataka watendaji
kujiona kuwa wao ni watu wakubwa katika vituo vya kazi na ni niwatumishi wa
Serikali na hivyo kutokubali kuendeshwa kisiasa hali ambyo itawafanya waweze
hata kuheshimika katika maeneo ya kazi.
“Ukimwona Mtendaji wa kata yupo sambamba na Diwani
wake katika mambo mbalimbali ya kazi ujue kuwa mtendaji huajiamini katika kazi
yake anayoifanya na kufanya kutokuwa na maamuzi ya msingi katika kazi
anazozifanya”, Alisema Mkuu wa Wilaya ya Kahama Benson Mpesya.
Pia aliwaasa kuwa na utaratubu wa kusomewa wananchi
wao mapato na matumizi kwa kile chocho wananchi wanachochangia katika mambo
mbalimbali katika kata zao hali ambayo itawapelekea wananchi kuwa na imani na
kazi wanazozifanya.
“Ninawaambia kuwa nyinyi watendaji ni marufuku
kuingia katika mradi mwingine bila ya kusoma mapato na matumizi kwa Wananchi
unaowaongoza jamii ya sasa ina mwamko mkubwa kwa sasa”, Alisema Mkuu huyo wa
Wilaya.
Pia alisema kuwa kunapokuwa na jambo lolote la
utekelezaji lazima litazamwe kwa makini ili kila mmoja asiweze kuathirika
katika shughuli zake anazozifanya hali ambayo itafanya kazi ya utawala bora
kufanyika bila ya wasiwasi wowote.
Katika kikao hicho cha maendeleo ya Wilaya mambo
mbalimbali yalizungumziwa hasa katika sekta mbalimbali kama vile Elimu maji na
Afya huku Kampuni ya Barrick nao wakielimisha washiriki kuhusu kujuhadhari na
matumizi ya kemikali ya Cynide
inayotumika katika kukamatia madini ya dhahabu.
mwisho
No comments: