sponsor

sponsor

Slider

Theme images by kelvinjay. Powered by Blogger.

Kimataifa Habari

habari

Habari Za Mastaa

Michezo

simulizi za kusisimua

» »Unlabelled » Wacheni kubaguana katika matumizi ya bwawa la maji



Na Mohab Dominick
        04 Nov,2013
            kahama
Wakulima na wafugaji katika kijiji cha Shunu kata ya Nyahanga wilaya ya Kahama mkoani Shinyanga wametakiwa kuacha kubaguana katika matumizi ya bwawa la maji lililopo katika kitongoji cha Mtakuja.

Wito huo umetolewa leo na mtendaji wa kata ya Nyahanga Nambo Ntaki wakati akizungumza na gazeti la nipashe  katika bwawa hilo lililofanyiwa ukarabati na kampuni ya CHICCO ya mjini Kahama ili liweze kuwasaidia wananchi hao.

Ntaki amesema siku za Nyuma kumekuwa na tetesi kuwa bwawa hilo ni kwa ajili ya wafugaji tu hali iliyozua mijadala mara kwa mara  katika mikutano ya wananchi na kwamba bwawa hilo ni kwa ajli ya wananchi
wote.

Sambamba na hayo ametoa wito kwa wananchi wa kijijiji cha shunu kuimarisha ulinzi katika bwawa hilo ikiwa ni pamoja na kuchangia
michango ya ukarabati wa bwawa hilo pasipo kuingiza itikadi za
kisiasa.

Naye mtendaji wa kijiji cha Shunu Benjamini Makelo ameishukuru kampuni ya CHICCO kwa kuwasaidia kukarabati bwawa hilo na amewaomba wazidi kujenga mahusiano mazuri hususan katika shughuli za maendeleo ya kijamii ukiwemo ujenzi wa zahanati ya kijiji unaoendelea.

Kwa upande wake meneja maeneo wa kampuni ya CHICCO Zhang Hao amesema kwa kampuni ya CHICCO itaendelea kushirikina na uongozi wa kata ya Nyahanga katika shughuli za maendeleo na kwamba maombi yaliyotolewa na mtendaji wa kijiji cha Shunu atayafikisha katika uongozi wa juu.

Kampuni ya ujenzi ya CHICCO leo imetoa msaada ya kukarabati bwawa la maji katika kijiji cha Shunu lililokuwa limebomolewa na mvua kubwa iliyonyesha mwanzoni mwa mwezi wanne mwaka huu hali iliyofanya bwawa hilo kushindwa kuhuifadhi maji.

MWISHO

«
Next
Newer Post
»
Previous
Older Post

No comments:

Leave a Reply