Na
Nzega
January 9,2014,
MBUNGE KUIBULUZA H/M
MAHAKAMANI.
KATIKA Hali isiyo ya kawaida
mbunge wa Jimbo la Nzega Dkt,Hamis Kigwangalla ameongoza maandamano na wananchi
zaidi ya 2000 wilayani Nzega ya kupinga maamuzi ya Baraza la madiwani la
Halmashauri ya wilaya kwa matumizi ya Fedha za Ushuru wa Huduma kutoka mgodi wa
dhahabu wa Resolute Bill 2.1.
Akihutubia mamia ya wananchi katika
viwanja vya maengesho ya magari akiwa
ameambatana na madiwana watano wanao muunga mkono alisema kuwa amepanga kuweka
zuio la matumizi ya fedha hizo katika mahakama Kuu ili suala hilo liweze
kupatiwa ufumbuzi wa msingi.
Alisema Halmashauri hiyo itafikishwa
mahakamani ili iweze kuzuiwa kupanga matumizi na maadhiumio ya Baraza hilo
ambalo aliliita lenye madiwani mizigo ambao hawana uwezo wa kupambanua mambo ya
msingi dhidi ya wananchi wao.
Hatua hiyo imetokea baada ya Baraza
la madiwani kuidhinisha fedha hizo zitumike katika kukamilisha miradi na kuibua
miradi ya maendeleo ya wananchi kwa kila kata huku wasimamizi wa kuu wa miradi
hiyo na kuibua kwa kushirikiana na wananchi wakiwa ni madiwani.
Baraza hilo lilithia kwa kupiga kura
za ndio 34 huku kura za madiwani ambao hawakuridhia na matumizi hayo ya pesa
wakiwa 5 pamoja na mbunge huyo hali ilipelekea Mbunge kutoka kikaoni.
Akiwahutubia wananchi Kigwangalla
alisema kuwa fedha hizo za ushuru wa huduma kutoka Resolute zikipelekwa kwenye
miradi kwa kila kata zitatafunwa na baadhi ya madiwani ambao hawana
nidham ya fedha na kuongeza kuwa fedha hizo hazita leta tija na matokea sahihi
kwa kukidhi kero za wananchi.
Mbunge huyo aliwaambia wananchi hao
kuwa vita hiyo anayo pigwa ni vita inayoanzia ndani ya chama cha mapinduzi huku
lawama kubwa akimtuhumu katibu wa chama cha mapinduzi CCM kajoro vyohoroka kwa
kuendesha mchakato wa kuwashinikiza madiwani kugawana fedha hizo kwa kila kata.
Alisema kuwa hatofika katika ofisi
ya chama hicho hadi pale katibu huyo wa chama atakapo hamishwa na kuongeza kuwa
hatofika katika ofisi za Halmashauri ya wilaya m,paka matumizi ya fedha hizo
yabadilishwe.
Vipaumbele vya mbunge huyo dhidi ya
fedha hizo ni ununuzi wa mitambo ya ujenzi wa Barabara vijijini ilikukidhi haja
za wananchi,ununuzi wa mtambo wa kuchimbia visima ilikukidhi kero ya maji
pamoja na kuanzisha Benk ya kijamii itakayo weza kukopesha wajasilia mali.
Alisema kuwa mapendekezo hayo
yalipitishwa toka vikao vya awari laikini baraza hilo lilipindisha kanuni za
baraza na kulazimisha kutoa maadhimio ya awari bila kufuata taratibu na kanuni.
Mbunge huyo aliwaita madiwani wote
waliopiga kura za pesa hizo zipelekwe kwenye miradi ya kata zao kuwa ni
madiwani mizigo katika Halmashauri zao na kuahidi kuwaambia wananchi wao dhidi
ya uzaifu wa hoja zao.
Awari ya hapo Diwani wa kata Nzega
Mjini Domick clement kizwa kupitia CUF alimpongeza mbunge huyo na kuwa pongeza
madiwani wa CCM walio muunga mkono mbunge huyo dhidi ya kupinga matumizi ya
fedha hizo.
Mbunge huyo aliongoza maadamano hadi
ofisi ya Mkuu wa wilaya ya Nzega huku wananchi wakiwa wamebeba ujumbe
mbalimbali dhidi ya fedha hizo na kuitaka serikali kusimamisha haraka matumizi
ya pesa hizo badala yake wafuate matakwa ya msingi yenye kutatua kero za
wananchi.
Mkuu wa wilaya ya Nzega Bituni
Msangi akipokea maandamano hayo na kuyajibu alisema kuwa ombi la wananchi hao
limepokelewa na ofisi yake na kuwaahidi kuyafanyia kazi huku akiomba utulivu na
amani idumu kwani suala hilo linafanyiwa kazi.
Mwisho.
No comments: