sponsor

sponsor

Slider

Theme images by kelvinjay. Powered by Blogger.

Kimataifa Habari

habari

Habari Za Mastaa

Michezo

simulizi za kusisimua

» »Unlabelled » MKURUGENZI AANGUSHA BONGE LA PATI KUWASHAWISHI MADIWANI KUPITISHA MAKISIO YA MAJETI 2014/2015Na 
 Mkurungezi wa halmashauri ya ushetu isabela chilumba akitoa tangazo katika ukumbi wa maarifa ya jamii ya kuwataka waandishi wa habari kuwacha vifaa vya kazi katika paty kama vile kamera na kamera za mnato

Kahama
Jan 14, 2014.
 

Katika hali ya kushangaza mkurungezi wa halmashauri ya ushetu wilayani kahama Isabela chilumba aangusha bonge la sherehe kwa lengo  la kuwashawishi madiwani wa halmashauri yake kupitisha makisio ya bajeti ya kiasi cha bilioni 32.5mwaka 2014/2015.
Katika sherehe hiyo ambapo vyombo vya habari havikurusiwa kuingia na vifaa vya kufanyia kazi  vikiwemo kamera na vifaa vingine vya kurekondia sauti kwa madai ya kuwa kilikuwa ni kubadilishana mawanzo Baina ya wakuu wa idara ,madiwani na kamati ya ulinzi na usalama ya wilaya ya kaham,
“Hata nyinyi   waandishi tunawaalika  katika Sherehe hiyo muhudhurie lakini msije mkaja na vifaa ya kufanyia kazi zenu kama kamera na vyombo vya kurekodia sauti hii ni shrehe ya kubadilishana na mawazo tuu”, Alisema Isabela Chilumba Mkurugenzi wa Halmashauri ya Ushetu.
Hata hivyo Mwandishi wa Gazeti la Nipashe alifanikiwa kuingia katika sherehe na kufanikiwa kuona baadhi ya Madiwani wakiwa katika makundi makundi wakijadili baadhi ya mambo ambayo iliashiria kuna baadhi ya mambo yalikuwa yakipangwa katika sherehe hiyo yalioashiria dalili za Rushwa kutoka Mkurugenzi huyo ili waweze kupitisha bajeti.
Halmashauri hiyo ya  Wilaya ya Ushetu katika kikao cha baraza la Madiwani kilichofanyika muda mchache kabla ya shrehe hiyo ilipanga kupitisha  makisio ya kutumia kiasi cha shilingi Bilioni 32.5 katika bajeti ya  kipindi cha mwaka 2014/2015 kwa ajili ya Mishahara kwa wafanyakazi na miradi mbalimbali ya maendeleo.

Mkurugenzi wa  Halmashauri ya Ushetu Isabela Chilumba alisema kuwa fedha hizo ni kwa ajili ya matumuizi ya kawaida na miradi mbalimbali ya maendeleo.

Alisema kuwa katika bajeti hiyo shilingi bilioni 30.7 ni ruzuku kutoka Serikali kuu ikiwa ni sambamba na wahisani mbalimbali ambapo ni sawa na punguzo la asilimia 11 ikilinganishwa na mwaka 2013/2014 ambapo makisio ilikuwa ni kiasi cha shilingi bilioni 39.3 ikiwa bilioni 37 ni ruzuku kutoka serikalini.

Chilumba aliendelea kusema kuwa katika bajeti ya mapato ya ndani Halmashauri yake imekisia kukusanya kiasi cha shilingi bilioni 1.8 kutoka katika vyanzo mbalimbali  vya mapato ya ndani  sawa na punguzo la silimia 21 ikilinganishwa na mwaka uliopita.

Ailisema kuwa baadhi ya vipaumbele katika bajeti hiyo ni pamoja na suala la Elimu, Afya na maji pamoja na miundombinu ya barabara pamoja na ujenzi wa Hospitali mpya ya Wilaya ya Ushetu ambayo kwa sasa haipo.

Mkurugenzi huyo aliendelea kusema kuwa katika mapato ya ndani ya Halamshauri ya Ushetu kwa kiasi kikubwa yanatokana na zao la Tumbaku ambalo kwa kipindi cha mwaka 2013/2014 makisio  ya zao hilo yalikuwa ni shilingi milioni 863.9 ambapo katika makusanyo Halmashauri hiyo ilipata kiasi cha shilingi bilioni 1.02 sawa na ongezeko la asilimia 118 ikiwa shilingi milioni 157.7

Hata hivyo katika uwasilishwaji wa makisio ya bajeti hiyo maadhi ya Madiwani wa Halmashauri waliishauri serikali kuangalia uwezekano wa kutotegemea sana ushuru wa zao la Tumbaku ambao ndio mkubwa kutokana na zao hilo kwa sasa kuwa katika wakati mgumu wa kupigwa vita.

“Tunaweza sisi kama Halmashauri kutafuta zao lingine mbadala la kuiingizia Halmashauri yetu mapato badala ya zao la Tumbaku ambalo siku likipigwa marufuku basi mapato yote yatakosekana na hivyo halmashauri kushindwa kujiendesha”,Dowa Makingi Diwani wa Kata ya Nyankende.

mwisho«
Next
Newer Post
»
Previous
Older Post

No comments:

Leave a Reply