Na
Kahama
Jan 13, 2013.
MAMLAKA ya Mapato (TRA) Wilayani Kahama Mkoani
Shinyanga imesema kuwa haitasita kuwachukulia hatua wafanyabiasha ambao
watakwepa kulipa mapato kwa mamlaka hiyo kwa mujibu wa sheria na taratibu
zinavyosema.
Hayo yalisemwa juzi na Meneja wa Mamlaka hiyo
Wilyani Kahama Peter Nkwabi wakati akiongea na Gazeti la nipashe juu ya baadhi ya wafanyabiashara Wilayani hapa
kuwa chanzo cha kupoteza mapato kwa mamlaka hiyo kwa kukwepa kulipa kodi.
Nkwabi alisema kuwa kuna baadhi ya wafanyabiashara
wamekuwa wakikwepa kulipa kodi huku wakisingizia kuwa biashara zao bado ndogo
hali ambayo hawapaswi kulipa kodi katika mamlaka hiyo.
“Wafanyabiashara wengi hasa katika Mji wa Kahama
wanahisi kuwa suala la kulipa kodi katika mamlaka hiyo siyo halali na kuwa
wanasema uongo wanapoulizwa juu ya kiasi cha fedha wanazingiza kwa siku na
kuipa mamlaka wakati mgumu katika kuwakadiria juu ya mapato yao wanayoingiza”,
Alisema Peter Nkwabi.
“Kwa mujibu
wa sheria za TRA maafisa wake wanatakiwa kukaa katika kila duka kuangalia
mfanyabiashara anauza kiasi gani kwa siku lakini wafanyabiashara hawa wamekuwa
wagumu kukaguliwa na ndio maana wanakuwa wakilalamika kwa kitu wasichokijua”,
Aliongeza Meneja huyo wa TRA Peter Nkwabi.
Nkwabi
alisema kwa sasa wao kama mamlaka hawatakubali kuona mamlaka hiyo inakosa
mapato kwani tumeazimia kwa wale wote watakaokwepa kulipa mapatao ya Serikali
tutawachulia hatua kwa mujibu wa sheria za Mamlaka husika zinavyosema
Aidha aliendelea kusema kuwa unakuta mfanyabiashara
unakudanganya juu ya mapato yake kwa siku na kuongeza kuwa mara nyingine
tunakuta magari makubwa yakishusha mizigo mikubwa na kutufanya tuyakubali
makadirio yake.
Kwa upande wao baadhi ya Wafanyabiashara mjini
Kahama walitoa malalamiko yao juu ya TRA kwa kusema kuwa maafisa wa Mamlaka
hiyo wamekuwa wakiwalazimisha kufungua droo zao na kuhesabu fedha ili wajue juu
ya mauzo yao kwa siku.
Pia walikataa kutumia mashine za (EFD ) mpya za
mamlaka hiyo kwa kusema kuwa wao hawawezi kuzitumia kwani elimu yao bado ni
ndogo ya kutumia mashine hizo huku wakitoa visingizio vya kukatikakatika kwa
umeme mara kwa mara kutawaathiri katika biashara zao.
Wafanyabishara hao waliazimia kuitisha mkutano
mwingine hivi karibuni kwa lengo la kujadili mambo hayo ikiwa ni sambamba na
kutoa maamuzi juu ya kumkataa mwenyekiti wa chemba ya wafanyabisha Mkuu wa
Wilaya mstaafu Meja Bahati Matala kwa kudai kuwa hawawezi kuongozwa na mtu
ambaye sii mfanyabiasha.
Mwisho
No comments: