Kahama
Jan 16, 2013.
BARRICK BUZWAGI YATUMIA MILIONI 43 KWA MWAKA KUSADIA
WANAFUNZI WASIOKUWA NA UWEZO KATIKA SHULE TATU WILAYANI KAHAMA
KAMPUNI ya Afican Barrick kupitia Mgodi wake wa
Buzwagi imetumia kiasi cha shilingi milioni 43.6 katika kusadia Wanafunzi wasiokuwa na uwezo vifaa
mbalimbali vya masomo katika shule tatu za sekondari zinazozunguka Mgodi huo
ikiwa ni sambamba na kuwalipia karo za masomo kwa kipindi mwaka 2013.
Kampuni hiyo kwa kupitia mradi wake wa Can Educate
ambao wafanyakazi wa migodi yake huchangia kwa lengo la kusadia Wanafunzi
tayari imekwishatoa msaada huo katika sekondari za Mwendakulima, Bugisha,
pamoja na Sekondari ya Nyasubi ambazo zipo jirani na Mgodi huo.
Akizungumza katika makabidhiano ya vifaa hivyo kwa
awamu ya mwisho mjini Kahama kwa wanafunzi wa sekondaro hizo Meneja Mahusiano
wa Mgodi huo huo Steve Kisakye alisema kuwa lengo la la Mgodi huo kusadia
wanafunzi hao ni katika nia ya kuboesha Elimu kwa wanafunzi.
Kisakye aliendelea kusema kuwa lengo jingine ni
katika kuhakikisha kuwa wanafunzi wanapata Elimu na kuongeza kuwa sio walio
kando ya Mgodi wa Buzwagi tu ilahata wale waliopo jirani na migodi ya North
Mara pamoja na Mgodi wa Tulawaka na Bulyanhulu.
Aidha Meneja mahusiano huyo alisema kuwa katika
Mgodi wa Bulyanhulu wamesadia jumla ya wanafunzi 900, Mgodi wa North Mara
Wanafunzi 200 wakati katika mgodi wa Buzwagi wamesadia wanafunzi 400 sambamba
na ukarabatio wa shule ununuzi wa madawati, na Elimu ya vyuo vikuu kwa
wanafunzi wanaofanya vizuri.
Kwa upande wake Meneja Mgodi wa Buzwagi Filbert
Rweyemamu alisema kuwa mgodi huo hautaacha kuwasadia wanafunzi hao hasa wasijiweza katika kutimiza ndoto zao
za baadaye ni hivyo kupata wasomi watakaoendesha migodi hiyo hapo siku za
baadaye.
Rweyemamu alisema kuwa pia kwa kugawa misaada hiyo
itakuwa ni changamoto kwa wanafunzi kufanya vizuri darasani na hata kupunguza
kwa kiasi Fulani suala la utoro kama lilikuwepo kwa wanafunzi kwa kuwa wana nyenzo za kusomea kwa
sasa.
Akitoa Shukrani kwa niaba ya Mkurugenzi wa
Halmashauri ya Mji wa Kahama Richard Msagati aliwataka wawekezaji hao kutokata
tama katika kusadia jamii ya kitanzania kwani kwa mgodi kuwa karibu imekuwa msaada mkubwa kwao na kwa Halmashauri
kwa ujumla.
Mgodi wa Dhahabu wa Buzwagi kupitia mradi huo wa Can
Educate imeshasaidia mambo mbalimbali ya kielimu katika shule hizo kwa mwaka
huu kama vile sale za shule kwa wanafunzi, sweta, kwa wanafunzi 400 huku
wasichana wakiwa 185 na wavuala 215 ikiwa ni sambamba na karo za shule milioni
nne Mwendakulima sekondari, milioni mbili Bugisha Sekondari na Nyasubi milioni
mbili huku jumla ikiwa ni shilingi milioni nane huku kwa mwaka wakitoa jumla ya
shilingi milioni 43.
Mwisho.
BAADHI YA WANAFUNZI WA SHULE ZA MWENDAKULIMA ,NYASUBI.NA BUNGISI WAMSIKILIZA MENEJA WA MGODI WA DHAHABU WA BUZWAGI JANA MJINI KAHAMA
WANAFUNZI WA SHULE YA SEKONDARI YA MWENDAKULIMA WAKISOMA RISALA KWA MGENI RASMI WA MGODI WA DHAHABU WA BUZWAGI MJINI KAHAMA
No comments: