sponsor

sponsor

Slider

Theme images by kelvinjay. Powered by Blogger.

Kimataifa Habari

habari

Habari Za Mastaa

Michezo

simulizi za kusisimua

» »Unlabelled » BARRICK YA WAFUNDA WAFANYABIASHARA WA MKOA WASHINYANGA




    Shinyanga
    Febr 24
 Meneja wa mgodi wa Buzwagi philbert Rweyemamu akitoa maada kwa wafanyabiashara wa mkoa wa shinyanga kwenye mkutano kushoto ni mkuu wa mkoa wa shinyanga Ally Rufunga .
 Mgeni Rasmi mkuu wa mkoa wa shinyanga All Rufunga katika mkutano wa wafanyabiashara wa mkoa wa shinyanga na migodi ya Buzwagi na Bulyanhulu  kwa kuwapatia fursa ya kufanya nao biashara .
 Afisa mahusiano wa maendeleo ya jamii wa mgodi wa buzwagi  Stephen kisakye hakiteta jambo na mkuu wa mkoa wa shinyanga Ally Rufunga wakati wa mkutano na wafanyabiashara wa mkoa wa shinyanga juu ya kufanya biashara na migodi ya Buzwagi na Bulyanhulu .
 Meneja wa Royal supermarket2008 William Matonange akitao maada juu ya kufanyabiashara na makampuni makubwa ya migodi ya Buzwagi na Bulyanhulu na wafanyabiashara wa mkoa wa shinyanga.
 Mwenye miwani ni Afisa maendeleo ya jamii  wa migodi wa Bulyanhulu  Abdahall mssika wakisikiliza maada mbalimbali kutoka kwa wafanyabiashara wa mkoa wa shinyanga
 Afisa maendeleo ya jamii mwenye tai moses msofe akiongea na katibu wa wafanyabiashara mkoa wa shinyanga juu ya kufanya shughuli na migodi hiyo ya Africa Barrick gold mine
 Baadhi ya wafanyabiashara wakisikiliza mada mbali mbali juu ya kufanyabiashara na migodi
 Meneja wa Royal supermarket2008 William matonange wakiteta jambo na mkuu wa mkoa wa shinyanga Ally Nassor Rufunga kabla ya kuanza mkutano na wafanyabiashara
 Afisa maendeleo ya jamii wa mgodi wa Bulyanhulu Abdahal mssika akimkaribisha mkuu wa mkoa wa shinyanga Ally Nassor Rufunga kabla ya kuanza mkutano na wafanyabiashara na migodi ya Africa Barrick gold mine mjini shinyanga
 Afisa mahusiano wa Buzwagi Blandina munghezi Akisikiliza mada mbalimbali zinazotolewa na wafanyabishara kwenye mkutano huo na migodi ya Buzwagi na Bulyanhulu mjini shinyanga
Mwenye suti kijivu na karatasi mkononi meneja wa maendeleo ya jamii wa mgodi wa Buzwagi Stephen kisakye akitoa maelezo kwa mkuu wa mkoa wa shinyanga Ally Nassor Rufunga kabla ya kuanza kwa mkutano na wafanyabiashara wa mkoa wa shinyanga .



KUENDESHA Biashara bila ya kufuata misingi ya Sheria, taratibu na kiwango cha juu cha maadili ni moja kati ya Changamoto zinazowakabili Wafanyabiashara Mkoani Shinyanga kupata fursa ya kufanya biashara na Migodi ya Barrick Tanzania.

Hayo yalisemwa juzi na Afisa kutoka katika kitengo cha Ugavi katika Migodi ya Afrikani Barrick gold Mine Dickson Liwumba katika kikao kilichowajumuisha Wafanyabiashara waliopo Mkoani Shinyanga na wale wanaofanya kazi na Migodi hiyo kutoka sehemu mbalimbali kanda ya ziwa.

Liwumba alisema kuwa mbali na Changamoto hiyo pia Wafanyabiashara wa Mkoa wa Shinyanga wamekuwa hawapati fursa hizo pia kutokana na  bidhaa zao kutokuwa na kiwango na kutomudu idadi ya vitu vinavyohitajika kwa wawekezaji hao.

Afisa huyo alisema kuwa pia ushirikiano baina ya Wafanyabiashara wa Mkoa wa Shinyanga na kutoridhika pia katika suala zima la kujiendeleza nalo ni tatizo kubwa hali ambayo inakuwa vigumu hata kuomba Zabuni katika makapuni hayo pindi zinapotokea.

Kwa upande wake Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga Ally Rufunga akifungua mkutano huo uliandaliwa na Kampuni ya African Barrick Gold Mine alisema kuwa Wafanyabiashara hasa wa Mkoa wa Shinyanga wanapaswa kujua kuwa wao bado wana fursa kubwa ya kufanya kazi na migodi hiyo miwili.

Alisema kuwa anawashukuru pia Uongozi wa Migodi hiyo miwili ya Buzwagi na Bulyanhulu kwa kufanya mkutano na kutoa Elimu kwa Wafanyabiashara hasa wa Mkoa wa Shinyanga katika kufuata Sheria na muda katika kuendesha biashara zao hasa katika maeneo ya wawekezaji wa Migodi.

Mkuu huyo wa Mkoa wa Shinyanga alisema kuwa Wawekezaji wanataka bidhaa zenye kiwango na kuongeza kuwa kwa kutumia Mkutano huo Wafanyabiashara wa Mkoa waShinyanga hawana budi kubadilika na kuongeza kuwa kama kuna masuala ya kiserikali yanayowasumbua basi ofisi yake ipo wazi kwa kutoa kutoa ushauri wa kibishara.

Pia Rufunga aliwaomba Kampuni hiyo kuwa na utaratibu wa kuendesha mikutano kama hiyo mara kwa mara kwa lengo la kutoa Elimu kwa Wafanyabiashara hao hali ambayo inaweza kuleta mabadiliko hasa kwa Wafanyabiashara wa Mkoa wa Shinyanga kuweza kuchangamkia fursa zilizopo katika migodi inayowazunguka.

Mkutano huo wa siku moja uliofanyika mjini Shinyanga ulijumuisha Wafanyabiashara kutoka Mkoa wa Shinyanga na wale ambao tayari walishaanza kufanya biashara na kampuni hiyo huku lengo kubwa likiwa ni kutoa Elimu kuhusu kuweza kupata fursa za kufanya biashara na Kampuni ya Barrick

mwisho

«
Next
Newer Post
»
Previous
Older Post

No comments:

Leave a Reply