sponsor

sponsor

Slider

Theme images by kelvinjay. Powered by Blogger.

Kimataifa Habari

habari

Habari Za Mastaa

Michezo

simulizi za kusisimua

» »Unlabelled » KAMPENI ZA UDIWANI KATA YA UBAGWE WANA CCM WAKATWA MAPANGA NA CHADEMA.MTENDAJI WA KATA HALI MBAYA

Kahama
Febr 5, 2014.

  

KAMPENI za uchaguzi mdogo wa Kiti cha Udiwani katika kata Ubagwe Wilayani Kahama Mkoani Shinyanga umeingia dosari baada ya watu wanaodhaniwa kuwa ni wafuasi wa Chama cha Demokrasia na Maendele (CHADEMA) kuvamia na kuwajeruhi vibaya wafuasi wa CCM kwa kuwajeruhi vibaya kwa kuwakata mapanga.

Akiongea katika Hspitali ya Wilaya ya Kahama alipolazwa Katibu Mwenezi wa CCM Wilaya ya Kahama Masood Melimeli alisema kuwa tukio hilo lilitokea majira ya saa moja na nusu usiku wakati wafuasi hao wa chama hicho wakitokea katika kijiji cha Ihata kwenda kwenda Itobola katika Kampeni.

Alisema kuwa walipofika katikakati ya Pori walikutana na gari ya CHADEMA aina ya Toyota land Cruser ikiongozwa na Mbunge wa Jimbo la Maswa Masahariki Sylivesta Kasulumbai na kuanza kuwashambulia kwa kutumia mapanga, Nondo pamoja na fimbo na kuwajeruhi  vibaya watu sita akiwemo dereva wa gari za CCM huku wengine wawili wakipotea kusikojulikana.

Waliojeruhiwa katika mapambano hayo ni pmaoja na Katibu Mwenezi wa CCM Masood Melimeli aliyeimia sehemu ya mkono na Bega, Ramadhani Salumu aliyepigwa panga la Mguu na Mkono, Sebastian Masonga aliyevunjwa Mkono wa kushoto, Dereva Charles Muhiga aliyejeruhiwa sehemu za kichwani, Mtendaji wa Kata ya Ubagwe Stephen Kimario aliyepigwa vibaya sehemu na kichwani na kupasuka na hali yake ni mbaya.

Melimeli alisema kuwa katika tukio hilo wafuasi wawili wa Chama hicho waliofahamaika kwa jina moja moja na Ismail na Samweli wao walipotea kusikojulikana na kutokana na kuona wenzao wakishambuliwa vibaya kwa kutumia vitu vyenye ncha kali vikiwemo Nondo pamoja na mapanga.

Kwa upande wake katibu Mwenezi wa CCM Mkoa wa Shinyanga Emanuel Mlimandago amelaani kitendo hicho na kusema kuwa  hiyo  siyo demokrasia ya kweli na kuongeza kuwa Watanzania wote hawanabudi kukilaani.

Katika vurugu hizo ambazo zinasadikiwa kufanywa na wafuasi wa Chadema, Mbunge wa Jimbo la Maswa mashariki Sylivesta kasulumbai anashikiliwa na jeshi la Polisi Wilaya ya Kahama kwa mahojiano zaidi kuhusu kufanyika kwa tukio hilo.

Nae Mwenyekiti wa TADEA Wilaya ya Kahama Charles Lubala akizungumzia kuhusu tuki hilo alisema kuwa mfuasi wa CHADEMA alivamia katika mkutano wa CCM na ndipo walipomkamata na kumuweka katika gari la CCM kwa lengo la kumpeleka katika kituo kidogo cha Polisi Bulungwa.

Hata hivyo baada ya kumuweka katika gari la CCM wafuasi wa chadema walipotangulia mbele na kuweka vizuizi barabarani na hivyo kusababisha vita hivyo kufanyika na kupelekea watu haoa sita kujeruhiwa huku hali ya Mtendaji wa kata hiyo ikiwa ni mbaya na amelazwa katika Hospitali ya Wilaya.

“Kwa kweli hizi kampeni zimekuwa kama  vita kwa sasa ni hatari na unapaswa kujihami kikamilifu kwani unaweza kupoteza maisha hivi hivi kwa ajili ya Kampeni hizi zinazoendelea hapa Ubagwe”, Alisema Mwenyekiti huyo wa TADEA Charle Lubala.

Hata hivyo katika kuonyesha kuwa kunaweza kutokea vurugu katika kata hiyo ambayo uchaguzi wake wa udiwani unatarajiwa kufanyika tarehe tisa mwezi huu vijana wa CCM walionekana kujiandaa vilivyo baada ya kuondoka kwenda katika kampeni hizo huku baadhi yao wakiwa wamesheni majambia.

Kampeni za Uchaguzi katika kata ya Ubagwe Wilayani Kahama Mkoani Shinyanga zinafanyika kufuatia aliyekuwa Diwani katika kata hiyo Richard Mndula kufariki Dunia mwaka jana huku kinyang’anyiro hicho kikiwahusisha wagombea watatu  kutoka katika  vyama vitatu vya CCM, TADEA pamoja na CHADEMA.

mwisho




 DEREVA WA GARI LA CCM CHARLES MHINGA HAKIWA HOI HOSPITAL YA WILAYA YA KAHAMA BAADA YA KUJIRUHIWA NA WAFASI WA CHADEMA
 MTENDAJI WA KATA YA UBAGWE  KIMARIO HAKIWA HOI HOSPTA L YA WILAYA YA KAHAMA
 MWENYEKITI WA WAZAZI WILAYANI KAHAMA IBRAHIMU KAN AKIMJULIA HALI KATIBU MUENEZI WA CCM WILAYA KAHAMA  MASOOD MELI MELI
 KATIBU MUENEZI WA CCM MKOA WA SHINYANGA EMMANUEL MALIYANDAGO,NA KATIBU MSAIDIZI WA CCM AZIZA WAKIWA HOSPITAL YA WILAYA NJE WODI  KUWAJULIA HALI WACCM WALIJERUHIWA NA WAFASI WA CHADEMA
 KATIBU MSAINDIZI WA CCM AZIZA AKIWA AMEJINAMIA KWA MAJOZI BAADA YA KUPATA HABARI YA WANA CCM WAKO HOI HOSPITALI

 MKURUNGEZI MTENDAJI WA HALMASHAURI YA USHETU ISABELA SHILUBA AKIWA NA KATIBU KATIBU WA CCM MKOA WA SHINYANGA HALIPOFIKA HOSPITALI YA WILAYA KUJUA HALI ZA MAJERUHI
 KATIBU MUENEZI WA CCM WILAYA YA KAHAMA MASOOD MELI MELI IKIWA WODINI
DEREVA WA CCM CHARLES MHINGA AKIONYESHA JERAHA LAKE LA KICHWA

«
Next
Newer Post
»
Previous
Older Post

No comments:

Leave a Reply