sponsor

sponsor

Slider

Theme images by kelvinjay. Powered by Blogger.

Kimataifa Habari

habari

Habari Za Mastaa

Michezo

simulizi za kusisimua

» »Unlabelled » UKATANAJI WA MAPANGA KATIKA MAMBO YA UCHAGUZI YAWATIA HOFU WALIMU KAHAMANa 
 MGENI RASM KWA NIABA YA MKUU WA WILAYA YA KAHAMA BENSONY MBESYA AKIVALISHWA SIKAFU KATIBU TAWALA FROLENCE MPETA KWENYE MKUTANO MKUU WA ROBO MWAKA WA CHAMA CHA WALIMU WILAYA YA KAHAMA( CWT)
 BAADHI YA WAJUMBE WA MKUTANO MKUU WA CHAMA CHA WALIMU WILAYA YA KAHAMA (CWT )
 KATIBU WA CHAMA CHA WALIMU MKOA WA SHINYANGA (CWT )MWENYE TISHIT YA JANO REHEMA SITTA
 MGENI RASM KATIBU TAWALA WA WILAYA YA KAHAMA FROLENCE MPETA AKIFUNGUA MKUTANO MKUU WA ROBO WA CHAMA CHA WALIMU WILAYA YA KAHAMA
 MGENI RASM KATIBU TAWALA MWENYE SUTI YA KIJIVU AKISALIMIANA NA KATIBU WA WALIMU WILAYA YA KAHAMA KEHA SAIMON KWENYE MKUTANO MKUU WA ROBO MWAKA WA CHAMA HICHO WA KUPATA MATUMIZI NA MAPATO YAO.
 WAJUMBE WA MKUTANO MKUU WA CHAMA CHA WALIMU( CWT) WILAYA YA KAHAMA WAKIMSIKILIZA KWA MAKINI MGENI RASM AMBAYE HAYUPO PICHANI KWENYE MKUTANO WAO WA ROBO MWAKA .
 MWENYEKITI WA CHAMA CHA WALIMU WILAYA YA KAHAMA( CWT) MWALIMU VICTOR TANDISE .AKIWAKALIBISHA WAJUMBE WA MKUTANO MKUU WA ROBO MWAKA WA MAPATO NA MATUMIZI
 MWENYEKITI WA (CWT) WILAYANI KAHAMA MWALIMU VICTOR TANDISE AKISISITIZA JAMBO LA HUFANYAJI KAZI WA WALIMU NA KUACHA KUNYANYASWA JUU YA HAKI ZAO .
 MJUMBE WA MKUTANO MKUU WA CHAMA CHA WALIMU AKIONGEA JUU YA MAPUJO YAO YA NAULI ZA LIKIZO NA KUPANDA MADARAJA YAO.
 MWENYEKITI WA CHAMA CHA WALIMU MWENYE TISHIT NYEUPE AKIONGOZANA NA MGENI RASM KATIBU TAWALA FROLENCE MPETA WAKIGIA NDANI YA UKUMBI WA MKUTANO KABLA KUANZA KWA KIKAO HICHO
 KATIBU WA CWT MKOA WA SHINYANGA REHEMA SITTA AKISISITIZA UZALENDO JUU YA HAKI ZAO
 WAJUMBE WA MKUTANO MKUU WA CWT WA HALMASHAURI TATU ZA MSALALA USHETU NA MJI WAKIMSIKILIZA MGENI RASM KWENYE MKUTANO WA ROBO MWAKA WA MAPATO NA MATUMIZI 
 MWENYEKITI WA CHAMA CHA WALIMU MKOA WA SHINYANGA GEORGE NYANGUSU

 KATIBU WA CWT WILAYA YA KAHAMA KEHA SAIMON AKISOMA TAARIFA YA MAPATO NA MATUMIZI YA ROBO MWAKA YA CHAMA CHAO CHA WALIMU WILAYA KAHAMA
Kahama
Febr 16, 2014.

UKATANAJI WA MAPANGA KATIKA MAMBO YA UCHAGUZI YAWATIA HOFU WALIMU KAHAMA

KUFUATIA hali ya vurugu ya kukatana Mapanga kwa Wafuasi wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) na wale wa CCM  iliyojitokeza katika Kampeni za uchaguzi Mdogo wa kiti cha udiwani katika kata ya Ubagwe Wilayani Kahama Mkaoni Shinyanga imewatia wasiwasi Walimu katika kusimamia uchaguzi Uchaguzi Mkuu ujao.

Wasiwasi huo ulitolewa juzi na Mwenyekiti wa Chama cha Walimu Mkoa wa Shinyanga George Nyangusu katika kikao cha Mkutano Mkuu wa Chama cha Walimu Wilaya ya Kahama kilichofanyika mjini hapa na kujumuisha wanachama wake wa Wilaya za Ushetu, Kahama Mjini na Msalala.

Katika Mkutano huo ambao ulijumuisha zaidi ya Walimu 333, Mwenyekiti huyo alisema kuwa vitendo vilivyofanywa na wafuasi wa vyama hivyo viwili imeleta sura mpya kwa Walimu ambao kwa kiasi kikubwa ndio wasimamizi wa chaguzi mbalimbali zinazoendeshwa na  Serikali.

“Sisi Walimu hali hiyo mpaka kufikia sasa inatutisha katika zoezi zima za kushiriki katika uchaguzi Mkuu ujao kutokana na vitendo vya ukataji wa mapanga yaliotokea hasa katika kata ya Ubagwe na kwa ili serikali iliangalie kwa umakini lisijirudie tena”, Alisema George Nyangusu.

Aidha Nyangusu alisema kuwa inasikitisha kwa Wilaya ya Kahama yenye rasilimali nyingi ikiwa ni pamoja na misutu kuona katika shule zake za msingi bado kuna kundi kubwa la Wanafunzi wanaofundishwa wakiwa wamekaa chini na kuongeza kuwa hali hiyo ni hatari kwa taifa la kesho.

Akisoma Risala ya Chama hicho Katibu wa Chama cha Walimu Wilaya ya  Kahama
Simon Keha alisema kuwa Walimu wanakabiliwa na Changamoto nyingi katika maeneo yao ya kazi ikiwa ni pamoja na utekelezaji wa ratiba za ukamilishaji za masomo ambapo wanafunzi wanatoka muda wa saa 12 tofauti na maeneo mengine.

Keha aliendelea kusema kuwa Changamoto nyingine ni pamoja na lugha mbaya zinazotolewa  kutoka kwa Watendaji wa Serikali  ikiwa sambamba na kucheleweshewa madai mbambali wanayokuwa wakidai kama fedha za uhamisho katika Halmashauri husika.

Kwa upande wake Mgeni Rasmi katika Mkutano huo kwa niaba ya Mkuu wa Wilaya ya Kahama Benson Mpesya, Katibu Tawala wa Wilaya ya Kahama Frolence Mpeta alisema kuwa Serikali inamtengemea Mwalimu katika masuala mbalimbali  ikiwa sambamba nay ale ya Uchaguzi Mkuu.

Mpeta alisema kuwa Suala la Walimu kupewa fedha za uhamisho kwenda katika kituo kingine lipo ndani ya uwezo wao na kuongeza kuwa atahakikisha kuwa masuala hayo kwa kushirikiana na Mkuu wa Wilaya yanafanyiwa kazi haraka iwezekanavyo kwani kwa kufanya hivyo hivyo kunaweza kuwapa Walimu morali ya kufanya kazi.

 Mwisho

«
Next
Newer Post
»
Previous
Older Post

No comments:

Leave a Reply