sponsor

sponsor

Slider

Theme images by kelvinjay. Powered by Blogger.

Kimataifa Habari

habari

Habari Za Mastaa

Michezo

simulizi za kusisimua

» »Unlabelled » WATENDAJI WA WIZARA YA NISHATI NA MADINI WATAKIWA KUTOKAA MAOFISINI



Na  Mohab Dominick
 Baadhi ya wachimbaji wadogo katika lashi ya nyangalata wilayani kahama mkoa shinyanga
 wachimbaji wadogo wakiosha mchanga hunaosadikiwa kuwa na dhahabu katika kijiji cha nyangalata wilayani kahama mkoani shinyanga  

Kahama
Febr 28,2014.

WATENDAJI WA WIZARA YA NISHATI NA MADINI WATAKIWA KUTOKAA MAOFISINI

WATENDAJI wa Wizara ya Niashati na Madini waliopewa Dhamana ya kusimamia sheria za Wachimbaji wadogo hapa Nchini wametakiwa kutokaa maofisini badala yake wazunguke kwa wachimbaji wadogo  kwa madhumuni ya kutoa Elimu kwao juu uchimbaji wa kufuata sheria.

Hayo yalisemwa juzi na Makamu Mwenyekiti wa Chama cha Wachimbaji wadogo Mkoa wa Shinyanga Nicodemus Majambe wakati akiongea na Mwandishi wa habari hizi juu ya vikwazo wanavyovipata Wachimbaji wadogo hapa nchini katika kupata maeneo ya Uchimbaji.

Majabe alisema kuwa Wachimnbaji wadogo hawana Elimu juu ya kupata maeneo ya uchimbaji wa Madini na kuongeza kuwa kama maoafisa wa Madini wasingekaaa maofisini basi kusingekuwa na migogoro yeyote juu ya kupata maeneo ya Uchimbaji.

Alisema kuwa katika meneo ya Uchimbaji wa Madini Wakuu wa Wilaya wamekuwa wakipta kazi ya kutoaa Elimu ya uchimbaji katika maeneo hayo kazi ambayo ilitakiwa kutolewa na maoafisa wa Madini wa Sehemu husika.

Makamu Mwenyekiti huyo alisema kuwa katika Mkutano waliokaa na Waziri wa Niashati na Madini Mjini Dodoma walikubali kuwa na ushirikiano mkubwa baina ya Viongozi wa Wachimbaji wadogo na Watendaji wa Wizara ya madini kwa ujumla.

Pia alisema kuwa urasimu uliopo kati ya Watendaji wa Wizara ya Madini na Nishati Tanzania ndio unaosababisha kuwepo migogoro mingi baina ya Wachimbaji wadogo na Makampuni makubwa ya uchimbaji.

“Kuna kesi nyingi ambazo  zipo baina ya Wachimbaji wadogo na Makampuni makubwa ya uwekezaji  zinazosababishwa na watendaji wa Wizara hiyo katika sehemu mbalimbali hapa nchini Waziri Mwenye dhamana na kuwa hana taarifa juu  Migogoro hiyo ambayo  inaleta mvutano mkubwa baina yapande hizo mbili”, Alisema Nicodemus Majabe.

Aidha alisema kuwa baadhi ya migogoro hiyo ni pale wachimbaji wadogo wanapoomba leseni za maeneo ya kuchimba lakini  wamekuwa wakipewa maeneo tofauti na y ale waliomba huku yale ya awali wakipewa wawekezaji wenye uwezo.

“Kuna maeneo kama yale ya Ny’angwale, Mwazimba, Kishapu na Mengine mengi katika Wilaya ya Kahama amabayo yaliombwa na Wachimbaji wadogo kwa ajili ya kufanya shughuli za uchimbaji lakini maeneo hayo walipewa wawekezaji wakubwa”, Alisisitiza Makamu Mwenyekiti huyo.

Makamu Mwenyekiti huyo alimuomba Naibu Waziri anayehusika na kitengo cha Madini Stephen Masele kujitahidi katika kuondoa migogoro hiyo ambayo kwa kiasi kikubwa imekuwa ni kero kwa Wachimbaji wadogo na Wawekezaji wa migodi na Serikali kwa ujumla.

mwisho


«
Next
Newer Post
»
Previous
Older Post

No comments:

Leave a Reply