sponsor

sponsor

Slider

Theme images by kelvinjay. Powered by Blogger.

Kimataifa Habari

habari

Habari Za Mastaa

Michezo

simulizi za kusisimua

» »Unlabelled » HALMASHAURI YA USHETU NA MSALALA WAVUTANA KUHUSU MRAHABA WA BULYANHULU.



Na  Mohab Dominick
Kahama
March 25, 2014.

HALMASHAURI YA USHETU NA MSALALA WAVUTANA  KUHUSU MRAHABA WA BULYANHULU.



Mkurungezi wa Halmashauri ya msalala Patrick karangwa akitoa maelezo juu ya mrahaba wa kuhusu mgodi wa dhahabu wa bulyanhulu kwenye kikao cha dharura cha madiwani 

 Eneo la mgodi wa Dhahabu wa buzwagi mjini kahama





HALMASHAURI mpya za Msalala na Ushetu Wilayani Kahama Mkoani Shinyanga juzi zimevutana kuhusu fedha za mapunjo zilizotolewa na Mgodi wa Bulyanhulu pamoja na Ushuru wa zao la Tumbaku kufuatia Halmashauri iliyokuwa mama ya Wilaya ya Kahama kufa na kuzaliwa kwa Halamsahuri hizo.

Katika kikao cha dharura cha Baraza la Madiwani wa Halmashauri ya Msalala kilichohudhuriwa na Mkuu wa Wilaya ya Kahama Benson Mpesya na Katibu Tawala wa Mkoa wa Shinyanga Anselim Tarimo ilishuhudia Madiwani hao wakigoma kutoa kiwango cha shilingi milioni 610 katika shilingi bilioni 1.4 zilizotolewa na Mgodi wa Bulyanhulu kama mapunjo.

Mgodi huo wa Dhahabu wa Bulyanhulu ulitoa kiasi hicho cha fedha kwa malengo ya kugawana nusu kwa nusu fedha hizo baada ya ile iliyokuwa Halmashauri ya Wilaya ya Kahama kufa na kuzaa Halmashauri hizo mbili za Ushetu na Msalala.

Akisoma taarifa ya mrejesho wa Mgawanyo wa fedha hizo za mapato ya ndani kutoka katika Mgodi wa African Barrick Gold Bulyanhulu Mkurugenzi wa Halmashauri ya Msalala Patrick Karangwa alisema kuwa katika kikao cha kamati ya fedha kilichokaa tarehe 27/1/2014 walijadili taarifa ya fedha hizo na kufikia maagizo.

Alisema baadhi ya maagizo walifikia ni Mkurugenzi wa Halmashauri ya Ushetu kufuatilia malipo ya Ushuru ya zao la Tumbaku kwa mwaka 2012/2013 wa iliyokuwa Halmashauri ya Wilaya ya Kahama ambao pia unastahili kugawanywa kwa Halmashauri zote mbili za Ushetu na Masalala.

Hata hivyo Karangwa alisema kuwa baada ya ufuatiliaji uligundua kuwa mapato ya Ushuru wa zao oa Tumbaku  kwa mwaka huo ulikuwa ni kiasi cha shilingi milioni 738.6 ambapo fedha hizo zilitakiwa kugawanywa kwa Halmashauri zote mbili.

Alisema Tarehe 05/2/2014 Halmashauri ya Wilaya ya Msalala ilihamisha kiasi cha fedha cha shilingi milioni 240.6 kwenda Halmashuri ya Ushetu  baada ya kutoa mgawanyo wa mapato ya tumbaku kutoka katika mgawo wa shilingi milioni 610 kwenye fedha kutoka Barrick Bulyanhulu.

Hata hivyo Halmashauri ya Wilaya ushetu ilikataa fedha hizo na hivyo kuzuia fedha za matumizi kutoka serikali kwenda Halmashauri ya Msalala ili kufidia fedha zilizokatwa hali ambayo ilizua mgogoro mkubwa baina ya Walimu na Mkurugenzi wa Ushetu Isabela Chilumba.

Hata hivyo katika kikao hicho kilichodumu kwa muda wa masaa sita kiliisha baada makubaliano chini ya Mkuu wa Wilaya Benson Mpesya na Katibu tawala Mkoa wa Shinyanga Anselim Tarimo kuunda tume kwa ajili kufuatilia fedha hizo pamoja na nyingine zilizopaswa kugawanywa baada ya iliyokuwa Halmashauri ya Wilaya Kahama kufa na kuzaa Halmashauri hizo.

mwisho

«
Next
Newer Post
»
Previous
Older Post

No comments:

Leave a Reply