sponsor

sponsor

Slider

Theme images by kelvinjay. Powered by Blogger.

Kimataifa Habari

habari

Habari Za Mastaa

Michezo

simulizi za kusisimua

» »Unlabelled » NANE WAFARIKI DUNIA BAADA YA KUANGUKIWA NA VIFUSI WAKICHIMBA DHAHABU KAHAMA

Na Mohab Dominick
   March 16,2014
          Kahama

NANE WAFARIKI DUNIA BAADA YA KUANGUKIWA NA VIFUSI WAKICHIMBA DHAHABU KAHAMA

Watu 8 wamefariki Dunia  na moja kunusurika  katika  machimbo  Madogo ya dhahabu katika kijiji cha kalole na Nyangalaya kata ya lunguya  wilayani kahama mkoani shinyanga baada ya kuangukiwa na vifusi katika mashimo waliokuwa wakichimba.

Akiongea na Waandishi wa Habari juu ya tukio hilo Mtendaji wa kijiji cha kalole Furaha mashamba ,alisema kuwa watu saba walikufa katika machimbo ya Kalole huku mmoja akifariki katika machimbo ya Nyangalata na hivyo kufikia idadi hiyo.

Mashamba alisema kuwa matukio hayo yalitokea juzi  juzi majira ya saa 5 usiku ambapo wachimbaji hao wadogo  katika machimbo hayo walifukiwa na udongo wa dhahabu katika mashimo walikuwa wakichimba.

Afisa Mtendaji huyo wa kijiji alizidi kusema kuwa wanakijiji  hao katika matukio hayo waliweza walishirikiana ili kuweza kuwaokoa wachimbaji hao hao baada ya tukio lakini ilishindikana na hivyo kufanikiwa kutoa miili   saba na moja akiwa hai na kukimbizwa kituo cha Afya Lunguya kwa matibabu zaidi .

Adhia  mtendaji huyo  aliwataja waliofariki dunia kuwa ni Mandogo Kibasi Kiaka (26) msukuma mkazi wa kalole ,Juma Malingaya miaka( 30) msukuma mkazi wa kalole ,Charles Iheyolo miaka (21)msukuma mkazi wa kalole ,Roma Masolwa miaka( 26)msukama mkazi wa kalole ,Juma John miaka( 33)msukuma mkazi wa kalole ,Paul Jemes miaka (24) msukuma mkazi wa kalole ,Ngaleba Kacheyekele miaka (24) na Michael Pius miaka (43)mkazi wa morogoro kabila mpongolo ambaye alinusurika,

Akifafanua zaidi Mtendaji  alisema kuwa chanzo cha ajali hiyo kuwa ni mashimo hayo kutokuwa na usalama wa kutosha na kuingiliwa na maji chini ya mashimo hayo kutokana na mvua za masika zinazoendelea kunyesha Wilayani hapa .

 Aidha Mtendaji  Furaha alisema kuwa maeneo haya yalishapigwa marufuku lakini wamekuwa wakiyavamia mara kwa mara hilo na kuongeza kuwa suala hilo  limekiwa ni tatizo sana kwa wachimbaji wadogo wadogo katika maeneo mbalimbali hapa nchini.

Kwa upande wake Mjiolojia wa  Madini wilayani kahama  Amir Chande alisema kuwa maeneo haya katika kijiji cha kalole walishayafunga kutokana na maeno haya kuwa ni hatari kwa usalama wa wachimbaji na  wamekuwa wakinyavamia mara kwa mara na kusababisha vifo vya mara kwa mara.

“Kuanzia sasa ni  marufuku kwa Wachimbaji kuchimba katika maeneo hayo hadi hapo Serikali itakapotoa maelekezo juu ya ni maeneo gani wanayotakiwa Wachimbaji wadogokuchimba kwa usalama wao na kufuata sheria na taratibu za uchimbaji’,Alisema Jiolojia huyo.

hapa nyinyi mpo kimakosa na kwa sababu hakuna mwenye leseni hapa ya uchimbaji wa madini kwa hiyo sasa ni makosa kufanya kazi hii ya uchimbaji na kuanzia sasa machimbo  tunayafunga kwa usalama wenu”, Alisema  chande ”

Aidha afisa huyo alizidi kufafanua kuwa ofisi yetu ipo wazi kwa kila mtu anayeteka leseni ya uchimbaji na siyo kuvamia maeneo ya  makampuni nyenye leseni  na kuongeza kuwa  mtu kuomba leseni ya uchimbaji wa madini mahali popote hapa Tanzania kwa maeneo ambayo tayari yana leseni za watu .


Afisa Mjolojia wa Madini wilayani kahama Amir chande Alijishika kidevu Akipewa maelezo na mtendaji wa kijij Furaha mashamba , ajali ya kufunikwa kwa watu nane katika machimbo madogo ya Dhahabu  katika kijiji cha  kalole
 Baadhi ya wananchi wakisubiri kutambua milii ya ndugu zao walifariki kwa kuangukiwa na udogo wa machimbo ya dhahabu katika kijiji cha kalole
 Baadhi ya wachimbaji wakiendelea kufukuwa mili ya jamaa zao walifukiwa na udogo ambapo urefu wa mashimo hayo ni zaidi ya meta saba toka juu ya ardhi


 Hii  ndiyo shimo ambalo watu nane walikuwemo ambapo saba walifariki Dunia  moja kunusurika katika ajali hiyo
 Afisa mjliojia wa madini Amir chande mwenye jackt la jano akitolea maelekezo juu ya uchimbaji wa Dhahabu eneo hilo ambapo wamepinga marufuku shughuli za uchimbaji huo mara moja
Baadhi ya wachimbaji wakiendelea kutafuta mili ambayo bado ipo chini

«
Next
Newer Post
»
Previous
Older Post

No comments:

Leave a Reply