Na Mohab Dominick
Shinyanga.
March 20, 2014
SERIKALI
YATENGA BILION 40.1 KWA AJILI YA KUSAMBAZA MAJI KATIKA VIJIJI SHINYANGA
SERIKAli imetenga
shilingi Billion 40.18 zitakazotumika kusambaza huduma ya maji katika
Vijiji 100 kutoka mradi wa maji ya ziwa Victoria kwenda wilaya nne
za mikoa ya Shinyanga na Mwanza, Imeelezwa.
Hayo
yameelezwa na Mkurugenzi wa Mamlaka ya maji safi na mazingira mjini Shinyanga
(SHUWASA) Mhandisi Sylvester Mahole wakati wa ufunguzi wa maadhimisho ya wiki
ya maji Mkoani hapa, jana
Mhandisi
Mahole alisema Miradi hiyo ambayo ni ya awamu ya pili inatarajiwa kuanza
kujengwa julai mwaka huu na inakadiliwa kukamilika juni 2019 na ujenzi wake
unatekelezwa na Serikali kwa kushirikiana na wadau wa maendeleo ya sekta ya
maji nchini.
Mahole
alisema jumla ya vijiji 150 kutoka wilaya za Kahama Shinyanga na Msalala Mkoani
Shinyanga pamoja na wilaya za Kwimba na Misungwi Mkoani Mwanza vimeainishwa
kupatiwa huduma ya maji ya bomba kutoka mradi wa maji ya ziwa Victoria.
Alisema
awali mpango huo una lengo la kusambaza huduma ya maji katika
vijiji 100 ambapo utekelezaji wake utaanza na vijiji 20 kwa kila
halmashauri na shughuli za upanuzi wa mtandao wa usambazaji maji
kutoka mradi wa maji ya ziwa Victoria kwenda katika vijiji 100 utajengwa kwa
kipindi cha miaka mitano.
Akihutubia
mkutano wa hadhara katika uzinduzi wa maadhimisho ya wiki ya maji
uliofanyika katika kijiji cha Bubinza wilaya ya Kishapu Mkoani hapa Mkuu
wa Mkoa wa Shinyanga Ally Rufunga alisema asilimia 51 ya wakazi wa
Mkoa wa Shinyanga vijijini hupata huduma ya majisafi na asilimia
58.5 kwa wakazi wa mijini hupata huduma hiyo.
Rufunga
alisema katika mipango ya muda mrefu miji ya Isaka na Kagongwa inategemewa
kunufaika na mpango wa kutoa maji ya ziwa Victoria kupeleka katika miji ya
Tabora, Nzega na Igunga ambapo hivi sasa usanifu unaendelea.
Mwisho.
No comments: