Watumishi wa utawala katika chama cha walimu Tanzania Kanda ya
magharibi wametakiwa kuwa faraja kwa walimu wanapofika ofisini kusikilizwa
matatizo yao, hali ambayo itawafanya kujisikia vizuri katika huduma zitolewazo
na chama hicho
Changamoto hiyo imetolewa mjini Kahama na mwenyekiti wa Chama cha
walimu Tanzania tawi la Kahama Victor Tandise wakati akifunga kikao cha
siku mbili cha watumishi hao kanda ya magharibi yenye mikoa minne ya Kigoma ,
shinyanga Simiyu na Tabora kilicho fanyika mjini Kahama.
Katika kikao hicho kilicho washillikisha makatibu wa mikoa na
wilaya pamoja na makatibu muktasi wao, Tandise amesema ili walimu kuwaweka kwenye
faraja ni lazima wapate huduma nzuri ya mapokezi katika ofisi za chama ambazo
ziko nchi nzima.
Aidha Tandise amesema kuna baadhi ya waajiri kama wakurugenzi
katika halmashauri ni wakorofi ambao huwakorofisha waalimu wakati wa kudai
maslahi yao, hivyo huwa changanya kiasi ambacho ofisi za vyama ndio iwe faraja
kwao.
Kabla ya hapo mwenyekiti wa kikao hicho ambae pia ni katibu CWT
mkoa wa Shinyanga Bi Rehema Sitta, amesema watumishi hao katika siku mbili
walizokaa wamejifunza mbinu mbalimbali ya kutoa huduma kwa walimu ingawa pia
wamepitia mkataba wa hali bora ya kazi zao za kila siku na kufanyia marekebisho.
Kikao hicho pia kimeipitisha wilaya ya Kahama kuwa ndio kituo cha
kufanyia vikao vyao kwa watumishi hao kutoka kanda hiyo ya magharibi, yenye mikoa
hiyo mine.
Na Mohab Dominick-kahama
Na Mohab Dominick-kahama
No comments: