mkurungezi wa clouds fm ruge mutahaba akitoa maelekezo juu ya fursa tufanikiwe pamoja katika ukumbi wa hotel ya niteshi mjini kahama .
msani wa sinema za bongo movie( bad boy )ibrahimu mbwana wakiwa na miliki wa blog ya Malunde kadama mwenye shati nyeusi katika ukumbi wa niteshi mjini kahama .
msani marufu wasiti almasi akiwa na mkurungezi wa sanaa wa afrikani seven mosha kwenye semina ya fursa ya tufanikiwe pamoja kati ya mgodi wa dhahabu wa buzwagi na african barrick gold mjini kahama .
baadhi ya washiriki wa semina ya fursa ya tufanikiwe pamoja wakiwa katika ukumbi wa nitesha.
baadhi ya washiriki wa semina ya fursa ya tufanikiwe pamoja na clouds fm na mgodi wa buzwagi african barrick gold mjini kahama wakisikiliza maoni mbalimbali kwa washiriki .
baadhi ya wandaji wa sinema mjini mwenye tisheti issa mbwana wakiwa wakibadilisha mawanzo katika senima ya fursa ya tufanikiwe pamoja kati ya mgodi wa dhahabu wa buzwagi na clouds fm mjini kahama .
mwenye shati ya misitali mkono mirefu moja wa toa fursa toka clouds fm raymond mtani akiwa na kikudi cha upendo sanaa cha mjini kahama wakibadilishana mwanzo juu ya fursa ya tufanikiwe pamoja .
mkurungezi wa clouds fm ruge mutahaba akitoa madaa juu ya kuwa na fursa ya tufanikiwe pamoja katika ukumbi wa niteshi hotel mjini kahama .
wasani marufu wa hapa nchini wasiti almasi na seven mosha wakisikiliza kwa makini muezeshaji hayupo pichani kwa fursa ya tufanikiwe pamoja kati ya mgodi wa dhahabu wa buzwagi na clouds fm mjini kahama.
afisa mahusiano wa mgodi wa dhahabu wa buzwagi wa african barrick gold dorothy bikurakule wakibadilishana mawanzo juu ya fursa ya tufanikiwe pamoja kati wajasiliamali na clouds fm na mgodi huo .
mkurungezi wa clouds fm ruge mutahaba akitoa maelekezo kw kijana ambaye ni msani chipukizi katika ukumbi wa niteshe hotel kwenye semina ya fursa ya tufanikiwe pamoja
mkurungezi wa clouds fm ruge mutahaba alisimama akitoa fursa ya tufanikiwe pamoja katika ukumbi wa nitesh hotel mjini kahama .
sikilizeni jamaani ndiyo maneno anayosema ruge mutahaba kwenye semina ya fusa ya tufanikiwe pamoja mjini kahama.
baadhi ya wadau wa fursa tufanikiwe pamoja .
mkurungezi wa clouds fm ruge mutahaba akisisitiza jambo juu ya fursa ya tufanikiwe pamoja /
wasani katika pozi kwenye fursa ya tufanikiwe pamoja /
majadiliano ya pamoja katika fusa ya tufanikiwe pamoja mjini kahama.
majadiliano ya pamoja akitolewa na raymon mtani je ya ukumbi wa niteshi hotel .
mazungumzo mwenye miwani ni msani seven mosha wakibadilisha mawanzo .
badhi ya vikundi mbali mbali wakijadiliana
majadiliano
fursa ya tufanikiwe pamoja
kaka hii ndiyo fursa tufanikiwe pamoja
majadiliano ya pamoja.
wadau wakisikiliza fursa ya tufanikiwe pamoja .
mkuu wa wilaya kiomboi yahaya navada akiwa na muandishi wa gazeti la habarileo raymond mihayo kwenye semina ya fursa ya tufanikiwe pamoja .
- wana habari wakiweka mambo sawa.
mjasilamali akisisitiza jambo juu ya fursa ya tufanikiwe pamoja kati ya clouds fm na mgodi wa dhahabu wa buzwagi african barrick gold katika ukumbi wa noteshi mjini kahama
Watanzania
wametakiwa kuchangamkia fursa zilizopo katika mazingira wanayoishi ili
kukabiliana na umaskini badala ya kulalamika kuwa hawana ajira wakati mwingine
kujikuta wakishinda vijiweni.
Hayo
yamesemwa jana na Meneja Mkuu mgodi wa dhahabu wa Buzwagi (ABG) Filbert
Rweyemamu wakati was Semina ya fursa "Tufanikiwe pamoja"ulioandaliwa
na kampuni hiyo kwa kushirikiana na Clouds Media Groups na kukutanisha makundi
mbalimbali ya wananchi wakiwemo wasanii,wajasiriamali,wakulima na wadau wa
maendeleo Wilayani Kahama.
Semina
hiyo ilikuwa na lengo la kuwaelimisha na kuwahamasisha wakazi wa
Kahama wakiwemo wajasiliamali wadogowadogo kuchangamkia fursa zilizopo kwenye
maeneo yao zizonaweza kuwapatia ama kunyanyua vipato vyao hususani katika
maeneo ya Migodi.
Rweyemamu alisema fursa inaanza
pale mtu anapotambua kuwa kuna fursa katika mazingira yake hivyo kuwaasa
wakazi wa Kahama waangalie katika mazingira yao nini kinahitajika ambacho
kinaweza kuwaingizia kipato ili kuondokana na umaskini katika jamii.
Alisema
kuwa nchi jirani za Uganda na Kenya zimepiga hatua kimaendeleo kutokana na
kwamba wananchi wake wamechangamkia fursa zilizopo kwenye maeneo yao ku
hivyo kuwataka watanzania kujenga uthubutu kuleta mapinduzi badala ya kuendelea
kulalamika kwamba ni maskini wakati watanzania wanazo akili za kuweza kufanya
mambo makubwa.
“Asilimia
kubwa ya watanzania ni vijana ,sisi African Barrick tumeungana na Clouds Media
Group kukusanya vijana ili kuwaeleza kuhusu fursa hizo,tunaamini fursa inaanza
hapo ulipo na tunawakaribisha kwenye migodi yetu,njooni tufanye
biashara”,alisema Filbert Rweyemamu.
“Ndugu
zangu mwenye macho haambiwi tazama,tunaacha mambo yanapita bila kuyafanyia
kazi,tujenge uthubutu,tusiseme sisi ni maskini wakati tunayo akili ya kufanyia
kazi mambo kadha wa kadha yaliyopo katika mazingira yetu”,alisisitiza
Rweyemamu.
Kwa
upande wake mgeni rasmi katika mkutano huo mkuu wa wilaya ya Iramba mkoani
Singida Yahaya Nawanda ,ambaye ana mradi wa ufugaji kuku katika wilaya yake
alisema juhudi inahitajika pale mtu anapotaka mafanikio hivyo kuwataka wananchi
kujituma katika kazi za mikono yao badala ya kukaa vijiweni kila wakati.
“Hakuna
serikali ambayo itakuletea maendeleo vijiweni,unayesubiri serikali ikuletee
pesa kijiweni kwako,utakaa hadi utachoka,tafuteni fursa katika maeneo
yenu,undeni vikundi vya kuwaletea kipato,fanya kazi za mikono yako utapata pesa
nyingi,mungu atakupa ridhiki kulingana na kazi zako",alisema Nawanda.
Naye mkurugenzi
mtendaji wa Clouds Media Group Ruge Mutahaba aliwaeleza wakazi wa Kahama
kuwa chochote kinachopatikana katika mazingira anayoishi binadamu ambacho
kunaweza kumfanya mtu kuingiza kipato ni fursa inayopaswa kuchangamkiwa haraka.
Mutahaba
aliongeza kuwa mji wa Kahama ambao unazungukwa na migodi ya dhahabu na sasa
unaendelea kwa kasi unazo fursa nyingi lakini wananchi hawajajua kuzitumia
hivyo kuwataka kuamka na kuanza kutengeneza pesa ili kujiiunua kiuchumi.
Hata
hivyo Mutahaba alisema ili kufikia malengo wananchi wanapaswa kujiamini na
kutoamini kushindwa huku akiongeza kuwa hakuna haja ya kutafuta kitu
kipya kwani fursa ziko nyingi waangalie namna ya kuziboresha ili kujipatia
kipato.
Mwisho
No comments: