MKUU WA JESHI LA POLIS (IGP )Ernest mangu akitoa taarifa juu ya uvamiwa kwa kituo cha polisi ushirombo mkoani Geita
kituo cha polisi ushirombo ambapo kilivamiwa na majambazi na kupoteza askari wawili na majambazi hao
Kamishina wa polisi Oporesheni ya mafunzo Paulo chagonja akitolea ufafanuzi suala la kuvamiwa kwa kituo cha polisi ushirombo mkoani Geita .
hiki ndiyo kituo cha zamani kabla ya kuhamia kwenye jengo jipya ambalo limetupiwa bomu la kutupa kwa mkono.
hiki ndiyo kituo kikubwa cha ushirombo ambacho kimetupiwa bomu la kutupa kwa mkono ambapo serikali lilijengwa kwa gharama kubwa kutokana na kukosa kituo hicho kwa kipindi kirefu wilayani hapa .
WATU
wanaodaiwa kuwa ni majambazi wamevamia Kituo Kikuu cha Polisi cha Wilaya ya
Bukombe kilichopo Ushirombo, mkoani Geita na kuua askari wawili na kuiba silaha
za moto.
Taarifa
za awali za tukio hilo zimethibitishwa na Kamishna wa Polisi, Operesheni na
Mafunzo, Paul Chagonja.
Akizungumza
na waandishi wa habari jana, alisema uvamizi huo unatajwa kufanywa majira ya
saa 9 usiku katika kituo hicho mkoani Geita, ambapo inadaiwa wahalifu hao ambao
idadi yao inakadiriwa kuwa zaidi ya kumi, walivamia kituo wakiwa na silaha za
kivita.
Alisema
mazingira ya tukio hilo inaelezwa kuwa majambazi hao walipofika kituoni hapo,
walitupa bomu la mkono katika chumba cha mashitaka na kusababisha vifo vya
askari wawili wenye namba G.2615 Dunstan Kimati na WP 7106 Uria Mwandiga huku
wawili wengine wakijeruhiwa.
“Walifika
katika kituo hicho wakiwa na silaha nzito za kivita, wamesababisha vifo vya
askari wawili, lakini wawili wengine wanaendelea na matibabu hospitalini,”
alisema Chagonja.
Alisema baada ya kuwaua na kuwajeruhi askari hao waliharibu
taa na kusababisha giza kutawala kituoni hapo, ambapo walivunja chumba cha
kuhifadhia silaha na kutoweka na baadhi ya silaha.
“Majambazi
hao walivunja na kuchukua baadhi ya silaha ambazo zilikuwepo kituoni hapo,
ambazo mpaka sasa idadi yake haijajulikana,” alisema Chagonja.
Chagonja
alisema idadi ya silaha hizo haijajulikana kutokana na operesheni mbalimbali
zilizokuwa zikiendelea wilayani humo, hivyo silaha zilikuwa zikiingia na
kutoka.
Chagonja
alisema, kutokana na tukio hilo Mkuu wa Jeshi la Polisi nchini (IGP) Ernest
Mangu yuko katika eneo la tukio akiwa amefuatana na Mkurugenzi wa Upelekezi na
Makosa ya Jinai (DCI) Isaya Mngulu na timu ya wataalamu wa upelelezi na
operesheni ili kuhakikisha wahusika wa tukio hilo wanakamatwa.
Hata
hivyo, aliwataka wananchi kuwa watulivu akisema Jeshi la Polisi litahakikisha
wahusika wa tukio hilo wanakamatwa na sheria kuchukua mkondo wake, lakini pia
aliwataka wananchi wenye taarifa muhimu zitakazosaidia kuwakamata wahalifu hao
wazitoe ili zifanyiwe kazi.
Kwa
mwaka huu tukio kama hilo la kuvamiwa kwa Kituo cha Polisi na kuuawa kwa askari
na majambazi kuchukua silaha ni la pili ambapo la kwanza lilitokea Juni, mwaka
huu katika Kituo kidogo cha Polisi cha Mkamba, wilayani Mkuranga Mkoa wa Pwani
ambako majambazi walimuua askari mmoja na kuwajeruhi wengine watatu na kupora
silaha tano zenye risasi ambazo ni SMG mbili na Shot gun tatu.
Hata
hivyo, wahalifu waliohusika na tukio hilo walikamatwa na kesi yao bado
inaendelea. Ingawa taarifa ya Chagonja haikueleza idadi ya silaha zilizoibwa,
taarifa za ndani ambazo blog hii inazo zinasema majambazi hao wameiba bunduki
kumi, risasi na mabomu ya mkono, kisha kutokomea.
Imeelezwa
kuwa baada ya kufika kituoni hapo, majambazi hao walizingira kituo hicho hadi
eneo la mapokezi na kuanza kuwamiminia risasi za moto askari waliokuwa zamu.
Mganga
Mkuu wa Wilaya ya Bukombe, Dk Honoratha Rutatinisibwa amekiri kupokea miili ya
askari wawili wa kike na kiume. Waliojeruhiwa wamefahamika kuwa ni askari
mwenye namba E.5831 David Ngupama Mwalugelwa aliyejeruhiwa kichwani na usoni na
kwamba ameumizwa vibaya sehemu za mdomo wake huku meno mawili yaking’oka.
Mwingine
ni Mohammed Hassan Kilomo aliyejeruhiwa kifuani na mguu wa kulia uliovunjika
mfupa kwa kupigwa risasi. Dk Rutatinisibwa alipoulizwa juu ya hali za majeruhi
hao, alisema ni mbaya na kwamba walilazimika kuwahamishia Hospitali ya Rufaa ya
Bugando, jijini Mwanza kwa matibabu zaidi.
Hilo
ni tukio la pili kwa askari wa kituo hicho kuuawa na majambazi ambapo Juni 28,
2009 kundi la majambazi saba wenye silaha za moto aina ya SMG, yaliteka magari
manne ya mizigo katika pori linalounganisha maeneo ya Runzewe, Matabi na
Buselesele lililopo Bukombe na kumuua askari Pascal wa Kituo hicho cha Polisi Bukombe.
MAJERUHI WANENA
Kilomo ambaye anapata matibabu Bugando alisimulia tukio hilo kuwa majambazi hao ambao idadi yao haijajulikana walivamia kituo hicho majira ya saa 8.45 usiku wa kuamkia jana wakiwa na bunduki na mabomu.
Alisema majambazi hao walishambulia kituo kwa kulipua bomu moja na kumimina risasi kadhaa kituoni, huku polisi watano waliokuwa kituoni wakijibizana nao kwa
risasi.
Alisema walizidiwa nguvu na majambazi hao, alipoteza fahamu na alipojitambua alijikutana Bugando. Kilomo alisema kuwa amejeruhiwa ubavuni, mguu wa kulia na mkono wa kushoto.
Blog ilishuhudia mguu wa Kilomo ukiwa umefungwa bandeji ngumu (PoP) na ubavu wa kulia ukiwa umefungwa bandeji, pia mkono wa kushoto umefungwa bandeji.
Mwenzake, Ngutama hali yake ni mbaya na amepoteza fahamu. Ngutama akiwa amefungwa bandeji kichwani na mkono wa kushoto.
Afisa Muuguzi Msaidizi wa Bugando, Elizabeth Edward, alisema kuwa majeruhi hao walipokelewa jana saa 7 mchana wakitokea Bukombe na hali ya Ngutama ilikuwa siyo nzuri. Alisema Kilomo hali yake inaendelea vizuri.
Alisema walizidiwa nguvu na majambazi hao, alipoteza fahamu na alipojitambua alijikutana Bugando. Kilomo alisema kuwa amejeruhiwa ubavuni, mguu wa kulia na mkono wa kushoto.
Blog ilishuhudia mguu wa Kilomo ukiwa umefungwa bandeji ngumu (PoP) na ubavu wa kulia ukiwa umefungwa bandeji, pia mkono wa kushoto umefungwa bandeji.
Mwenzake, Ngutama hali yake ni mbaya na amepoteza fahamu. Ngutama akiwa amefungwa bandeji kichwani na mkono wa kushoto.
Afisa Muuguzi Msaidizi wa Bugando, Elizabeth Edward, alisema kuwa majeruhi hao walipokelewa jana saa 7 mchana wakitokea Bukombe na hali ya Ngutama ilikuwa siyo nzuri. Alisema Kilomo hali yake inaendelea vizuri.
Mwisho
No comments: