Baadhi ya waandishi wa vyombo mbalimbali vya habari wakiwa katika ziara ya kutembelea migodi ya dhahabu na kamati ya mazingira ,ardhi nyumba na maendeleo katika mgodi wa buzwagi .
Mmoja wa watalamu wa kigeni akiwakaribisha baadhi ya wana habari katika ziara ya kamati ya mazingira .
kamati ya Bunge Ardhi maliasili na mazingira wakiwasili katika mgodi wa buzwagi wilayani kahama .
Mwenyekiti wa kamati ya Ardhi maliasili na mazingira mh James Lembeli.
Baadhi ya wajumbe wa kamati ya bunge ya ardhi maliasi na mazingira wakipewa maelezo toka kwa meneja wa mgodi wa buzwagi Filbert Rweyemamu Wakati kamati hiyo ilipotembelea mgodi huu .
Naibu waziri Ofisi ya makamu wa Rais mazingira (omr )ummy mwalimu mwenye miwani kifuani wakiwa katika ukumbi wa mgodi wa dhahabu wa buzwagi wakati kamati hiyo ilipotembelea mgodi huu .
Baadhi ya waandishi wa vyombo mbalimbali vya habari wakibadilisha mawanzo kabla ya kamati ya mazingira kuwasili katika mgodi huu.
Mmoja ya Dappa la kubeba mawe ya dhahabu nakupelekwa kwenye kinu cha kuvunja mawe ambapo gari hilo linauwenzo wa kubeba tani 150 za mawe hayo ya dhahabu .
Wajumbe wa kamati ya Ardhi maliasili na mazingira wakiangalia moja ya bwawa la kupokea maji toka ziwa victori ambapo bwawa hilo limejingwa kwa kiwango kikubwa .
Mmoja ya jengo la kituo cha Afya mwendakulima ambapo mgodi wa buzwagi hunafadhili kwa gharama nafuu.
Wajumbe wa kamati ya bunge Ardhi maliasili na mazingira wakitoka katika moja ya bwawa la sumu ya cyanide .
Hili ndiyo bwawa lenye sumu ya Cyanide ambalo limeifaziwa kwa umaki mkubwa katika eneo hilo .
Moja ya gari la kumwanga maji kwa ajili ya kuondoa vumbi la mchanga wa mawe ya dhahabu .
Mwenyekiti wa kamati ya Ardhi maliasili na mazingira Mh James Lembeli Akiongea na meneja wa mgodi wa buzwagi Filbert Rweyemamu na muandishi wa habari za mazingira Jacob Rusungu katika mgodi wa buzwagi .
Mwenyekiti wa kamati ya Ardhi mazingira Mh James Lembeli akiwa kwenye picha ya pamoja na muandishi wa habari za uchumi Herman Meza Mwenye miwani mnyeusi pamoja na wajumbe wa kamati hiyo .
Mwenyekiti wa kamati ya Ardhi maliasili na mazingira Mh James Lembeli Mwenye miwani Akipewa maelezo toka kwa meneja mkuu wa mgodi wa Buzwagi Firbert Rweyemamu mwenye karatas nyeupe .
Baadhi wa wajumbe wa kamati ya Ardhi maliasili na mazingira wakiwasili katika mgodi wa buzwagi .
Mmoja ya mtambo mkubwa wa kupokea maji toka ziwa victoria ambao hunaingiza maji hayo katika mgodi huu .
Meneja mkuu wa Mgodi wa Dhahabu Buzwagi Filbert Rweyemamu akizumgumza na wajumbe wa kamati ya bunge ya mazingira .
Wajumbe wa kamati ya bunge ya mazingira wakitoka maeneo kukangua sehemu mbalimbali za utunzaji wa mazingira katika mgodi huo.
Kamati ya Bunge ya ardhi,maliasili na mazingira imempa miezi
mitatu waziri wa nchi ofisi ya Makamu wa
Rais mazingira kufuatilia uzingatiaji wa sheria na kanuni za kuhifadhi
mazingira katika migodi yote nchini.
Mwenyekiti wa Kamati hiyo Mhe. James Lembeli alitoa maagizo
hayo kwa Waziri mwenye dhamana hiyo Mhe.Ummy Mwalimu mgodini
Buzwagi baada ya
kuhitimisha ziara ya kukagua migodi hiyo
kanda ya ziwa jana.
Mhe.Lembeli alisema kuwa hali ya usalama,hifadhi ya mazingira
na utekelezaji wa sheria na kanuni husika si nzuri kwa baadhi ya migodi nchini
jambo linalohatarisha usalama wa Binadamu na viumbe hai.
Hata hivyo alitoa sifa za kipekee kwa mgodi wa dhahabu wa
Buzwagi kwa namna ulivyopokea na kufanyia kazi maagizo yote ya Baraza la Taifa
la Mazingira (NEMC) hususani kulinda na kuhifadhi taka sumu zitokazo mgodini
zisiingie katika vyanzo vya maji.
Mhe.Lembeli alisema kuwa kamati yake imeridhika kuona kila
kitu kimewekwa kwa mpangilio bora kwa tahadhari na hali ya usalama ikiwamo
ulipuaji miamba na uhifadhi wa kemikali hatari zitumikazo kuchanjua dhahabu.
Akijibu hoja hiyo waziri mwenye dhamana hiyo katika ofisi ya
makamu wa Rais , Ummy Mwalimu aliahidi kutumia taasisi zote husika chini ya
ofisi yake ikiwamo NEMC,kukagua utekelezaji wa maagizo ya kamati hiyo ya Bunge.
“Mhe.Mwenyekiti ndani ya miezi mitatu tutafuatilia na kutoa
taarifa katika kamati hii kuhusu utekelezaji wa maagizo ya NEMC kwa migodi yote
nchini kuhakikisha inazingatia sheria na kanuni husika.”Alisema waziri Mwalimu.
Akijibu hoja za Kamati ya Bunge mkurugenzi mkuu wa NEMC
Eng.Bunaventure Baya alisema ameridhika namna mgodi wa Buzwagi ulivyotekeleza
maagizo ya Baraza hilo na hatimaye kupewa hati maalum ya kutambua jitihada
hizo.
Naye meneja mkuu wa mgodi huo Filbert Rweyemamu alisema kuwa
mgodi huo ulipokea malalamiko 36 toka kwa jamii inayozunguka mgodi huo na
kutatua 33 ambapo tatu zilizo baki zinaendelea kutafutiwa ufumbuzi.
MWISHO
No comments: