Kamanda wa polisi mkoa wa shinyanga justus kamugisha akitoa ufafanuzi juu ya mtoto paschal kutumbukia kwenye dimbwi la maji kwa wandishi wahabari.
Mtoto
aitwaye Paschal Bundala mwenye umri wa miaka 7 mkazi wa kata
ya Mwakitolyo wilaya ya Shinyanga vijijini amefariki dunia baada ya kutumbukia
kwenye dimbwi la maji.
Kwa
mujibu wa kamanda wa polisi mkoa wa Shinyanga Justus Kamugisha amesema tukio hilo
limetokea Novemba 15 mwaka huu ambapo mtoto huyo alifariki dunia papo hapo
baada ya kutumbukia kwenye dimbwi hilo akichunga ng’ombe.
Amesema
chanzo cha tukio hilo ni mtoto huyo kuteleza na kutumbukia kwenye dimbwi hilo.
No comments: