mwenyekiti wa Taasisi ya Mzalendo
Foundation, Khamisi Mgeja alipokuwa akizungumza na waandishi wa habari nyumbani
kwake mjini Kahama wakati akitoa salaam zake za kheri ya mwaka mpya wa 2015.
Ushauri huo umetolewa jana na
mwenyekiti wa Taasisi ya Mzalendo Foundation, Khamisi Mgeja alipokuwa
akizungumza na waandishi wa habari nyumbani kwake mjini Kahama wakati akitoa
salaam zake za kheri ya mwaka mpya wa 2015.
Mgeja alisema wakati taifa
likiingia katika kipindi kingine cha mwaka 2015 kuna umuhimu mkubwa wa mihimili
mikubwa mitatu hapa nchini ikatanguliza mbele suala la utekelezaji wa majukumu
yao kwa kuzingatia mipaka yake kama ilivyoainishwa ndani ya katiba ya Jamhuri
ya Muungano wa Tanzania ili kuepuka migongano isiyo ya lazima.
Alisema zipo dalili zilizoanza
kujitokeza kwa mihimili hiyo mikuu kuanza kuingiliana na kupingana katika
utekelezaji wa majukumu ya kila siku hali ambayo inaweza kuchangia kuharibu
mstakabali wa kiutawala na hivyo nchi kujikuta ikiingia katika mtikisiko
mkubwa.
Mwenyekiti huyo alisema katiba ya
Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ya mwaka 1977 toleo la 2005 imeainisha wazi
utekelezaji wa shughuli za mamlaka ya nchi katika ibara yake ya nne vifungu
vidogo vya (1) na (2) hivyo ni muhimu kwa kila mhimili ikaheshimu katiba hiyo
ya nchi.
“Kifungu kidogo cha (2) kinaeleza
kuwa, vyombo vyenye mamlaka ya utendaji vitakuwa ni serikali ya Jamhuri ya
Muungano na Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar, vyombo vyenye mamlaka ya
kutekeleza utoaji haki vitakuwa ni Mahakama ya Serikali ya Jamhuri ya Muungano
na;”
“Mahakama ya Serikali ya Mapinduzi
ya Zanzibar, na vyombo vyenye mamlaka ya kutunga sheria na kusimamia
utekelezaji wa shughuli za umma vitakuwa ni Bunge na Baraza la Wawakilishi,
utaona wazi kila mhimili umeainishiwa majukumu yake,” alieleza Mgeja.
Mgeja alitahadharisha migongano ya
kimihimili nchini kwamba isipochukuliwa tahadhari ya kila mhimili kuheshimu
eneo la mhimili mwingine kama ilivyowahi kutokea kipindi cha Spika wa bunge
lililopita la 2005/2010, Samwel Sitta na hivi karibuni katika bunge la juzi
lilipokuwa likijadili suala la akaunti ya Tegeta Escrow.
“Wakati wa kipindi cha Spika Sitta
(Samwel) tuliona ilivyotaka kutokea kwa mihimili kutaka kuingiliana na
kusababisha mtafaruku mkubwa, lakini nihivi karibuni katika bunge lilopita tulimsikia mama yenu Anne Makinda akilalamika
na kuwa wasihi wabunge wasimsababishie atakuwa
mgeni wanani katika mihimili mingine ,”
“Binafsi napenda kushauri wakati
tukiuanza mwaka huu wa 2015 na kuuaga mwaka 2014 ni vyema watanzania
tukahakikisha nchi yetu inaendelea kuwa na amani na utulivu tulionao, na
tuwaombe viongozi wetu wa madhehebu mbalimbali ya kidini waongeze maombi yao
katika kuiombea amani nchi yetu,” alieleza Mgeja.
Kwa upande mwingine Mgeja ambaye
pia ni mwenyekiti wa Chama cha Mapinduzi (CCM) mkoani Shinyanga ameishauri
serikali iangalie uwezekano wa kuanzisha vyuo maalumu vitakavyotoa mafunzo ya
kiuongozi ili kuiwezesha nchi iwe ikipata viongozi waliopitia mafunzo hayo.
Alisema kuanzishwa kwa vyuo hivyo
ni muhimu katika kipindi hiki na jambo la lazima kwa vile vitasaidia kupatikana
kwa viongozi waadilifu wenye kuheshimu miiko ya kiuongozi na kuelewa nini
wajibu wao kwa umma uliowachagua kuwaongoza.
“Ukweli mara nyingi tumekuwa
tukiwalaumu bure viongozi wetu tunaowakabidhi jukumu la kuongoza nafasi
mbalimbali za kiutawala , wengi wao tunawabebesha majukumu makubwa kuliko uwezo
walionao, uongozi siyo jambo la kufanyia majaribio, nchi kuwa na viongozi ambao
hawajaandaliwa juu ya utekelezaji wa majukumu yao kama viongozi, ni majanga, ni
muhimu wakaandaliwa,” alieleza Mgeja.
Mwisho.
No comments: