Picha_MWILI WA MAREHEMU WAZIRI CELINA KOMBANI WAWASILI NCHINI,KUZIKWA SIKU YA JUMATATU MKOANI MOROGORO
Viongozi mbalimbali wakiwa katika uwanja wa ndege wa Mwalimu Julias
Nyerere jijini Dar es Salaam tayari kwa kuupokea mwili wa marehemu
Celina Kombani.
Wananchi wa mkoa wa Morogoro wamepokea kwa majonzi msiba wa aliyekuwa
waziri wa nchi ofisi ya rais menejimenti ya utumishi wa umma na mbunge
wa jimbo la Ulanga Bi, Celina Kombani mazishi yanatarajiwa kufanyika
Jumatatu wiki ijayo katika eneo la shamba lake lililopo Lukobe manispaa
ya Morogoro.
Wakizungumza nyumbani kwa marehemu wakazi wa Morogoro wameeleza
kusikitishwa na msiba huo ambapo wamesema marehemu alikuwa kipenzi cha
watu, mchapa kazi na kuwataka wakazi wa Morogoro hususani wa jimbo la
Ulanga kuwa wavumilivu kwa kupotelewa na kipenzi chao ambapo waziri huyo
alikuwa anagombea ubunge kwa awamu ya tatu kwa tiketi ya CCM katika
jimbo la Ulanga.
Wakizungumza kwa niaba ya familia kaka wa marehemu Martin Ombeshi na
mkwe wa marehemu Bw, Jeradi Mlenge wamesema wameupokea msiba huo kwa
masikitiko ambapo wameeleza mazishi yatafanyika mkoani Morogoro siku ya
Jumatatu shambani kwake Lukobe na msiba utapelekwa nyumbani kwao Mahenge
wilayani Ulanga mkoa wa Morogoro.
No comments: