By: Mohab Dominic
on 00:07
/
 |
Siku chache baada ya Mwenyekiti wa Chama cha Wananchi CUF, Prof. Lipumba kuwavua uanachama Wabunge wanane wa Viti Maalum kisha Spika Ndugai kuridhia uamuzi huo, leo July 27, 2017 Wabunge hao wamefungua kesi katika Mahakama Kuu ya Tanzania.
Wabunge hao wamefungua kesi hiyo iliyopewa namba 143/2017 kupitia Wakili wao Peter Kibatala lakini hata hivyo bado haijapangiwa Jaji huku Wabunge hao wakidai hawajapewa muda wa kujitetea.
Mbali na kufungua kesi katika Mahakama Kuu Tanzania, pia wamekata rufaa ndani ya Chama chao kupinga utekelezaji huo na kuiomba Mahakama isitishe utekelezaji wa uamuzi wa kufukuzwa Uanachama wao.
ULIPITWA? Prof. Lipumba baada ya Spika kuridhia Wabunge 8 kuvuliwa uanachama
|
Tag:
habari
matukio
MOHABMATUKIO.BLOGSPOT.COM's Admin
We are.., This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.
No comments: