sponsor

sponsor

Slider

Theme images by kelvinjay. Powered by Blogger.

Kimataifa Habari

habari

Habari Za Mastaa

Michezo

simulizi za kusisimua

» » » TANZANIA KUENDELEZA USHIRIKIANO WA KIULINZI NA INDIA-MAJALIWA


Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akifurahia jambo na Mkuu wa Majeshi wa India, Admiral  Sunil Lanba. (kushoto), na Mkuu wa Majeshi, Jenerali Venance Mabeyo Ofisini kwake jijini Dar es salaam Julai 28, 2017, ambapo walifanya mazungumzo ya kimahusiano baina ya mataifa hayo mawili.(PICHA NA OFISI YA WAZIRI MKUU)


NA OWM, DAR ES SALAAM
WAZIRI MKUU Kassim Majaliwa amesema Serikali ya Tanzania itaendeleza ushirikiano na Serikali ya India katika nyanja mbalimbali ikiwemo ya ulinzi.
Ametoa kauli leo (Ijumaa, Julai 28 , 2017) alipokutana na kufanya mazungumzo na Mkuu wa Majeshi wa India, Bw. Admiral Sunil Lanba jijini Dar es Salaam.
Waziri Mkuu amesema Tanzania na India ni nchini ambazo zina uhusiano mzuri na wa muda mrefu, ambapo ameahidi kwamba Serikali itaendelea kuudumisha.
Ushirikiano wa Tanzania na India ni wa kihistoria, hivyo tutauendeleza na kuudumisha. India tunashrikiana nao katika sekta za uchumi, afya, elimu na ulinzi.”
Waziri Mkuu ameishukuru Serikali ya India kwa ufadhili walioutoa kwa Tanzania  katika kuimarisha miradi ya maji kwenye mikoa mbalimbali nchini.
Pia Waziri Mkuu amewakaribisha raia wa India kuja kutembelea maeneo ya  utalii nchini ukiwemo mlima wa Kilimanjaro, mbuga za wanyama na visiwa vya Zanzibar.
Kwa upande wake, Mkuu wa Majeshi wa India, Bw. Lanba ameishukuru Serikali ya Tanzania kwa ushirikiano inaoutoa kwa Serikali ya India hususan katika masuala ya ulinzi.
Amesema wamefanya kikao na Mkuu wa Majeshi nchini Generali Venance Mabeyo ambapo katika mazungumzo yao wameweka mikakati ya kushirikiana katika kuimarisha ulinzi hususan maeneo ya mipakani pamoja na masuala ya mafunzo

Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akizungumza na Mkuu wa Majeshi wa India , Admiral Sunil Lanba  (kulia kwake) pamoja na ujumbe wake, Ofisini kwake jijini Dar es salaam Julai 28, 2017. Kushoto kwake ni Mkuu wa Majeshi, Jeneral Venace Mabeyo.
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akijadili jambo  na Mkuu wa Majeshi wa India, Admiral  Sunil Lanba (kulia) baada ya mazungumzo yao Ofisini kwa  Waziri Mkuu  jijini Dar es salaam Julai 28, 2017 . Wapili kulia ni Mkuu wa Majeshi Nchini, Jeneral Venance Mabeyo na kushoto ni Balozi wa India Nchini, Sandeep Arya
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa  akiwa katika picha ya pamoja na  Mkuu wa Majeshi wa India Admiral Sunil Lanba  (kulia kwake ) na Mkuu wa Majeshi nchini, Jeneral Venance mabeyo (kushoto kwake ) baada ya mazungumzo yao, Ofisini kwa Waziri Mkuu jijini Dar es salaam Julai 28, 2017. Kushoto ni Balozi wa India Nchini, Sandeep Arya.

«
Next
Newer Post
»
Previous
Older Post

No comments:

Leave a Reply