Na
Kahama
Des
22, 2013.
IIMEELEZWA
kuwa sababu kubwa ya Mbegu za Pamba za Quton kutoota ni kutokana na kampuni
hiyo kuchuka mbegu kwa Wakulima ambazo tayari zinakuwa zimetiliwa maji kwa
kiasi kikubwa badala ya kutumia zile ambazo zimetoka katika mashamba ya mbegu.
Hayo
yalibainika juzi wakati wa Madahalo kuhusu kilimo cha Pamba ulioandaliwa na
Shirika lisilo la kiserikali la kutetea na kuimarisha Demokrasia pamoja na
utawala Bora (ADLG) ambapo baadhi ya wakulima wa zap la Pamba walipata fursa ya
kuchangia.
Akiongea
kwa niaba ya Makapuni ya ununuzi wa zao la Pamba Wilayani Kahama Edson Peter
Mwakilishi kutoka kampuni ya NIDA textile alisema kuwa kampuni ya quton imekuwa
ikinunua mbegu za pamba kutoka wakulima badala ya kutoa katika mashamba darasa
ya mfano wanayotakiwa kulimwa.
Peter
alisema kuwa kwa mujibu wa Sheria msambazaji wa mbegu za Pamba anatakiwa kuwa
na Shamba darasa kwa ajili ya Mbegu za Pamba hali ambayo kampuni hiyo imekuwa
kinunua mbegu kutoka kwa wakulima ambazo tayari zinakuwa hazina ubora.
“Ukitaka
kuamini kuwa mbegu hizo hazina ubora hebu chukua mkasi na kasha zikate utaona
hali ya majimaji ambayo tayari inashirikua mbegu hizo zimeoza hali ambayo kwa
sasa imeleta mazozo mkubwa kwa wakulima wa Pamba kwani hazioti”, Alisema Edson
Peter mwakilishi kutoka kampuni ya NIDA Texitile.
Pamoja
mambo mengine yaliojadiliwa katika mdahalo huo ambao pia uliwajumuisha wakulima
wa zao la Pamba maafisa kilimo kutoka Halmashauri tatu za Ushetu, Msalala
pamoja na mji pia walijadili juu ya serikali kuona umuhimu wa kuifuta bodi ya
pamba kwa haina msaada kwa mkulima.
“Hivi
bodi ya pamba haina muda wake na kwa nini serikali isiifute bodi hiyo kwani
haitusaidii kwa chochote ni bora ikawa hata muda wa kuongoza ili watu wawe
wanabadilishana kwa nia ya kumuinua kulima wa Pamba”, Alisema Peter.
Mmoja
wa wakulima wa Pamba kutoka katika Wilayani hapa Maimuna Saidi alisema kutokana
na upungufu mkubwa wa maafisa ugani uliopo ni bora serikali ikatumia vijana
waliomaliza kidato cha nne mwaka uliopita ukawapa mafunzo ya muda mufupia kwa
nia ya kuwaelimisha wakulima wa Pamba juu ya zao hilo.
Alisema
kuwa kwa sasa kuna upungufu mkubwa wa maafisa ugani katika maeneo wanayolima
Pamba hali ambayo inafanya wakulima wengine kufikiria kujitoa katika kulima zao
la Pamba kwa kuwa wanaona kuwa zao hilo halina tija kwani wanatumia nguvu kubwa
kulima huku mafanikio yakiwa ni madogo
mwisho
No comments: