MTO MKUBWA HUNAOTENGANISHA ENEO LA MGODI WA DHAHABU WA RESOLUTE
WACHIMBAJI WADOGOWADOGO WAKISILIZA MKUTANO WA HADHARA
BAADHI YA WACHIMBAJI WAKISIKILZA MKUU WA WILAYA YA NZEGA KATIKA MKUTANO WA HADHARA
AFISA UPELELEZI WA WILAYA YA NZEGA AKIONYESHA MKUU WA WILAYA YA NZEGA SEHEMU AMBAYO ILIFUKIWA CHINI YA KAMATI YA ULINZI NA USALAMA
MWENYEKITI WA KIJIJI CHA NHOBOLA AKITOA MALALAMIKO YAKE KWA MKUU WA WILAYA YA NZEGA KATIKA MKUTANO WA HADHARA BITINI MSANGI KUHUSU KUFUKUNZWA KATIKA MAENEO YAO
mkuu wa wilaya ya nzega Bitini msangi Akiongea na wachimbaji wadogo dogo katika kijiji cha Nhobola wilayani nzega
Nzega
Jan 3, 2014.
WACHIMBAJI wa dogo wa Dhahabu katika
machimbo madogo ya mwanshina katika kijiji cha Nhobola wilayani Nzega Mkoani
Tabora,wameiomba serikali kuwapatia ridhaa ya kuchimba dhahabu pembezoni mwa
mgodi mkubwa wa dhahabu wa Resolute ili wakidhi mahitaji yao ya msingi.
Wakizungumza katika mkutano wa
kijiji mbele ya mkuu wa wilaya ya Nzega Bituni Msangi walisema kuwa
serikali kupitia waziri wa NishatI na madini wamewaomba kuwapatia ridhaa ya
kuendelea na shuguli hizo za uchimbaji wa dhahabu pembezoni mwa mgodi wa
resolute kwa kuwa mwekezaji huyo muda wake unaishia mwaka 2015.
Mwenyekiti wa wachimbaji hao Joseph
Mabondo alisema kuwa mgogoro uliopo kati ya serikali na wachimbaji ni kutokana
na wachimbaji kukosa eneo la kuchimba dhahabu huku wawekezaji hao wakiwa na
eneo kubwa ambalo halitumiki hali inayo sababisha wachimbaji hao wadogo kukosa
sehem ya kuchimba iliwajipatie ridhiki.
Joseph aliiomba serikali isikie
kilio hicho kikubwa cha wachimbaji hao ambapo ni wakazi wa pembezoni na mgodi
huo iliwaweze kupatiwa kibali cha kuchimba dhahabu kwa uhuru kama baadhi ya
sehem nyingine jinsi wa chimbaji wadogo wanavyo endelea na shuguli zao.
Alisema kuwa kitendo cha kuwa piga
marufuku na kuwafukuza katika machimbo hayo nikusababisha mahusiano mabaya kati
ya wachimbaji na serikali na kuongeza kuwa wachimbaji hao wana haki ya kupewa
nafasi ya kuchimba ili kukidhi mahitaji yao ikiwa na kukuza uchumi wa ndani ya
wilaya hiyo.
‘’sisi siyo wakimbizi ndani ya nchi
hii ni wazawa kabisa tuna muomba waziri husika na naibu wake masele watusaidie
suala hili ili tuweze kujikidhi mahitaji yetu mambo ya kukimbizana na
kufukuzana sio vizuri serikali tutizameni kwa macho mawili na sisi tunufaike na
rasilimali zetu’’,alisema Joseph mabondo.
Alisema kuwa kwa sasa kuna baadhi ya
wawekezaji wamekuwa wakimiliki maeneo makubwa huku wakiwa hawayatumii katika
shughuli zao za uchimbaji hali ambayo kwa wachimbaji wadogo wakipewa maeneo
hayo wanaweza kuyaendeza kwa haraka zaidi.
‘Mwekezaji huyo wa mgodi wa Resolute
muda wake unaisha mwakani 2015 na kwa sasa hakuna shughuli zozote za uzalishaji
zinazoendelea katika mgodi huo mkwani hili eno lililobaki tusipewe sisi
wachimbaji wadogo tulio katika jirani na mgodi huu “Alisema Mwenyekiti huyo.
Kwa upande wake Mkuu wa Wilaya ya
Nzega Bitini Msangi alisema kuwa kuwa kilio cha Wachimbaji wadogo katika eneo
hilo amekisikia na kuhaidi kuwa suala hilo atalifanyia kazi yeye kwa kushirikiana na
kamati ya ulinzi na usalama ya Wilaya ya nzega huku lengo kubwa likiwa ni
kumshawishi mwekezaji wa Mgodi huo kuwapa eneo hilo wachimbaji wadogo ili
kuweza kulifanyia kazi katika shughuli za uchimbaji.
mwisho
No comments: