Jeshi
la Polisi limeendelea na kamatakamata ya wapinzani wa vyama vinavyounda
Ukawa katika maeneo mbalimbali likieleza sababu tofauti za kijinai
zinazohusishwa na masuala ya kisiasa.
Mpaka sasa wabunge wa upinzani waliokamatwa ni; Halima Mdee (Kawe),
Mwita Waitara (Ukonga) na Peter Lijualikali (Kilombero), wote wa Chadema
na baadhi ya madiwani wa chama hicho katika Jiji la Dar es Salaam.
Vilevile, imeelezwa kuwa Mbunge wa Ubungo (Chadema), Saed Kubenea alikuwa anatafutwa kuunguanishwa na wenzake.
Pia, baadhi ya wanasiasa wa CUF Zanzibar wamekamatwa na kuhojiwa kwa
madai ya kuwatusi viongozi wa Serikali ya Mapinduzi Zanzibar (SMZ).
Viongozi wa CUF waliohojiwa na polisi mpaka sasa ni Mkurugenzi wa
Mipango na Uchaguzi, Omar Ali Shehe na Kiongozi wa Mkakati wa Ushindi,
Mohamed Sultan Mugheir ‘Eddy Riyami’ ambaye yuko nje kwa dhamana.
Mbali na viongozi hao, Naibu Katibu Mkuu wa CUF, Nassor Ahmed Mazrui
jana amepatiwa barua ya wito na Polisi Zanzibar ikielezwa kuna mambo
yanamhusu.
Hii ni mara ya pili kwa Mazrui kuitwa polisi tangu kufutwa kwa uchaguzi
wa Oktoba 25, huku CUF ikidai kuwa huo ni mwendelezo wa mkakati maalumu
dhidi ya viongozi wa chama hicho.
Jana, Kaimu Mkurugenzi wa Habari na Uhusiano wa Umma wa CUF, Maalim
Hamad Masoud Hamad alidai kuwa hatua hiyo ni utekelezaji wa maagizo ya
kisiasa ya kutaka kumkamata kila kiongozi wa juu wa CUF kuelekea
uchaguzi wa marudio.
“Kwa viongozi wa CUF hili halishangazi, nahisi ingelikuwa ni hatua ya
kushangaza sana iwapo wanaoitwa kuhojiwa na polisi ni viongozi wa vyama
vingine.
"Sisi upande wetu hili ni jambo la kawaida mno na watu wasishangae,” alisema.
Mazrui ambaye pia alikuwa Waziri wa Biashara na Uwekezaji, ametakiwa
kuripoti Makao Makuu ya Polisi, Ofisi ya Upelelezi Ziwani mjini hapa
kesho saa 2.00 asubuhi na kuonana na mkurugenzi wa makosa ya jinai
Zanzibar.
Polisi Zanzibar imethibitisha kuwapo wito huo ikisema kuna mambo muhimu yanayomhusu mwanasiasa huyo.
habari
Habari Za Mastaa
Michezo
simulizi za kusisimua
MOHABMATUKIO.BLOGSPOT.COM's Admin
We are.., This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
Popular Post
-
Mwanamke mwenye umri wa miaka 60 aliyekatwa sehemu zake za siri (nyeti)Akiwa wodi katika hospital ya mkoa wa Tabora . MME AK...
-
DUKA LA KISASA LA DAWA MUHIMU BAMA PHARMACY LILPO MJINI KAHAMA MAJENGO KAMA LIVYO DR HERY MUGA AKITOA MAELENZO YA DAWA KWA MTEJA WAKE ...
No comments: