MKUU WA WILAYA YA KAHAMA VITA KAWAWA HAKUTANA NA WAFANYABIASHARA NA KUTOA BEI ELEKEZI YA SUKARI 2200 KWA KILO
by Mohab Dominic-
0
Mkuu wa wilaya ya kahama Vita kawawa picha hii alikuwa katika kikao cha wadau wa maji mjini kahama hivi karibuni
KUTOKANA na agizo la Rais John Magufuli la kuwasaka wafanyabiashara wa jumla wanaoficha sukari waiuze kwa Wananchi kwa bei elekezi ya Serikali, Jeshi la Polisi wilayani Kahama mkoani Shinyanga limefanya upekuzi katika baadhi ya maghala ya kuhifadhia sukari na kuwabaini baadhi ya Wafanyabiashra wanne wanajihusisha na kazi hiyo.
Kwa mijibu wa Rais John Magufuli alitoa agizo ikiwa ni sambamba na Wafanyabishara hao wa rejareja kuuza kwa bei iliyopangwa na Serikali ya Shilingi 1,800 wakati wafanyabiashara hao wa maduka wamekuwa wakiuza Bidhaa hiyo kwa bei ya juu marambili ya ile ambayo walitakiwa kuwauzia Wafanyabiashara wa rejareja.
Mkuu wa wilaya ya kahama vita kawawa hatoa bei elekezi kwa wafanyabiasha wa kahama kuuza sukari kwa bei ya 2200 kwa kilo